HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 06, 2013

Benki ya Exim yatunukiwa tuzo ya utunzaji bora wa mazingira mwaka 2013

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (Kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant (kulia) wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani katika viwanja vya Zakhem Mbagala Jumatano. (Na Mpiga Picha Wetu)
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (Kushoto) akimkabidhi kombe Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant (kulia) baada ya benki yake kutunikiwa tuzo ya utunzaji bora wa mazingira katika kipengele cha taasisi za fedha katika Tuzo za Mazingira Manispaa ya Ilala mwaka 2013. 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (wa pili ushoto) akimkabidhi kombe Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant (kulia) baada ya benki yake kutunikiwa tuzo ya utunzaji bora wa mazingira katika kipengele cha taasisi za fedha katika Tuzo za Mazingira Manispaa ya Ilala mwaka 2013. Akishuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Benki ya Exim mara baada ya kuikabidhi benki hiyo kombe baada ya kuibuka washindi katika kipengele cha taasisi za fedha katika Tuzo za Mazingira Manispaa ya Ilala mwaka 2013. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant (kulia) akionyesha cheti walichoshinda benki yake katika kutambua mchango wa benki hiyo kwenye utunzanji wa mazingira wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani 2013 jijini Dar es Salaam Jumatano. Katika ni Kaimu Meneja Masoko Anita Goshashy. 

Na Mwandishi Wetu


BENKI ya Exim imeibuka mshindi wa jumla kwa taasisi za fedha kwenye Tuzo za Mazingira zilizoandaliwa na Manispaa ya Ilala kwa Mwaka 2013.

 Tuzo hizo zinalenga kutambua mchango ya taasisi mbali mbali nchini katika utunzaji wa mazingira. Sherehe za utoaji wa tuzo hizo ilifanyika katika viwanja wa Zakhem, Mbagala na kuandaliwa na Wilaya ya Temeke ikiwa sehemu ya kuhadhimisha Siku ya Mazingira Duniani iliyoambatana ka kauli mbinu ya “Fikiri, Kula, Tunza”.


Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki ambaye alikuwa mgeni rasmi aliitahadharisha jamii kutunza mazingira wanayoishi ili kuwa na miradi endelevu.

“Mahali popote ambapo mazingira yameharibiwa hata uzalishaji wa chakula na mazao ya biashara utapungua siku hadi siku,” alisema. Alisema kuwa mkoa wa Dar es Salaam unachangamoto changamoto mbali
mbali katika masuala ya utunzaji mazingira zikiwemo usimamizi hafifu wa  sheria ndogo ndogo za hifadhi ya mazingira. “Kuna watu wanakiuka na wengine wanagomea lakini mkumbuke mnavofanya
hivyo mnajijengea maisha duni.

 Sheria hizi zinazowekwa naomba sana mzisimamie kwa manufaa ya taifa letu.

“Hatuna budi kutii sheria hizi bila shuluti na tukifanya hivyo Dar es Salaam yetu itakuwa sehemu nzuri sana pa kuishi,” aliongeza. Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant mara baada
ya kupokea tuzo hiyo alibainisha mikakati na jitihada za benki yake za kuendelea kuunga mkono kampeni mbali mbali za utunzaji mazingira nchi nzima.

Grant alisema kuwa kuna umuhimu kwa wadau wote kushirikiana kwa pamoja ili kuongeza nguvu katika utunzaji wa mazingira hali ambayo itasaidia kuongeza mapinduzi ya uchumi wa kijani (green economy) ili kuboresha maisha ya jamii na kupunguza mazingira hatarishi kwa ujumla.

“Benki ya Exim itaendelea  kuunga mkono jitihada za mapinduzi ya
uchumi wa kijani. Tunahitaji kuiacha sayari ikiwa na mazingira
endelevu kwa vizazi vijavyo.

“Mabadiliko makubwa yanatakiwa kufanwa haraka kama tunakitaji kupiga
hatua kweli. Lazima matendo yetu na maamuzi ya kimazingira tunayofanya
yalete mabadiliko ya kijamii na kiuchumi katika maisha ya kila mmoja
wetu nchini,” aliongeza Grant.

No comments:

Post a Comment

Pages