HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 06, 2013

CHANETA WAMPATA KATIBU MKUU

Na Elizabeth John
CHAMA cha Netibali Tanzania (CHANETA), kimemteua Katibu Mkuu wa muda, Dk. Maimuna Mrisha ambaye atafanya kazi kwa mujibu wa katiba ya chama hicho kwa kipindi cha miezi sita.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CHANETA, Annie Kibira, alisema katika kikao kilichowakutanisha kamati ya utendaji Juni Mosi walimteua katibu hiyo ambaye watafanya kazi pamoja hadi Desemba mwaka huu.

Aidha, Kibira alizitaka timu ambazo zitashiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki, kuthibitisha na kukamilisha taratibu zote kabla ya Juni 10.

“Klabu ambazo zitashiriki michuano hiyo ambayo itafanyika Nairobi Kenya, kuanzia Julai 13 hadi 20 ni Filbert Bayi, JKT Mbweni na Jeshi Stars,” alisema.

Mbali na hayo, Kibira alisema Jini 2 CHANETA na CHANEZA walikutana kisiwani Zanzibar, wajumbe 20 walihudhulia kikao hicho ambapo makubaliano na maazimio ya pamoja yalipitishwa kwa utekelezaji.

Kibira alitaja mambo ambayo yalijadiliwa katika kikao hicho na yanatakiwa kufanyiwa kazi na vyama hivyo kuwa ni pamoja na Utambulisho wa vyama kimataifa, Uwakilishi katika mikutano ya kimataifa, Mawasiliano na vyama vya kimataifa, Aina ya mashindano ya kimataifa yanayohitaji ushiriki wa pamoja.

Mengine ni mafunzo ya ndani na ya kimataifa, mafunzo ya kimataifa nje ya nchi, Ada za vyama kwa ulipaji wa pamoja, Miradi ya pamoja, Misaada ya kutosha kutoka vyama vya kimataifa, Uteuzi wa mwalimu wa timu za taifa za muungano, Uteuzi wa viongozi wa timu za taifa za muungano, Uteuzi wa timu za taifa za muungano, Ulipaji wa gharama za timu za taifa na muungano.

Mengine ni Ulipaji wa gharama za walimu na viongozi wa timu za taifa za muungano, Mawasiliano baina ya CHANETA na CHANEZA, Usimamizi na utekelezaji wa makubaliano, pamoja na Marekebisho ya makubaliano.


Aliongeza kuwa makampuni au taasisi zinakaribishwa kutumia mchezo wa Netiboli kutangaza bidhaa na huduma zao ikiwa ni pamoja na kujenga viwanja vya mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

Pages