Na Mwandishi Wetu
MREMBO Marieta Boniface juzi usiku alifanikiwa kutwaa taji la Redd’s Miss Chang’ombe, katika kinyang’anyiro kilichokuwa kikali kilichofanyika kwenye viwanja vya TCC Club, vilivyopo Chang’ombe, Dar es Salaam.
Marieta alifanikiwa kuwashinda warembo wengine 12 walioshiriki katika kinyang’anyiro hicho ambacho kilikuwa na upinzani mkali.
Kutokana na ushindi huo, Marieta alizawadiwa pikipiki yenye thamani ya Sh milioni 1.5 ambayo ilitolewa na wadhamini wenza Kampuni ya Kishen Enterprises Ltd.
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu aliyekuwa mgeni rasmi ndiye aliyemkabidhi zawadi hiyo na kusema amefurahishwa kwa kiasi kikubwa na shindano hilo na yupo tayari kulisaidia zaidi.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa taji, Marieta alisema anaamini kwa dhati atafanikiwa kufika mbali zaidi kwani amedhamiria kuhakikisha anaibeba Chang’ombe katika shindano la Redd’s Miss Tanzania.
Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.
No comments:
Post a Comment