HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 16, 2013

Serikali inatekeleza mpango upi! MKUKUTA au wa Miaka Mitano?

Na Bryceson Mathias
KWA muda mrefu sasa; Serikali imekuwa haieleweki ni Mpang gani inatekeleza ambao inaweza kujivunia kuwa umeifikisha mahali fulani kati ya MKUKUTA uliotoka Nje na Mpango wa miaka Mitano wa Rais Jakaya Kikwete.
Hata vipaumbele (Priorities) kimsingi vimekuwa havieleweki kiasi cha kuonekana hiki kimefanikiwa kwa kiasi gani! Bali imekuwa ikigusagusa leo Elimu, Kesho Afya, Kilimo, Miundo mbinu na sasa Nishati, lakini vyote hatuoni ufanisi na Tija yake.
Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania(MKUKUTA), kwa sasa umekuwa kama Mpango wa Kuchota Uchumi na Kuongeza Umaskini Tanzania, kwa sababu utekelezaji wake hauoneshi tija halisi ambayo inaweza kujivuniwa kuwa haya ndiyo mafanikio yake kwa Taifa na wananchi wake.
Kwa mfano; Hata katika Bajeti hii 2013/14, Serikali bado haijaonesha Nia dhabiti ya kupunguza matumizi yake, bali kila mwaka inazidi kuongezeka ikilinganishwa na Mwaka uliopita, ambapo Bilio Tatu zimeongezeka (Bil. 18/-) toka kwenye Bil.15/- za Bajeti ya mwaka uliopita 2012/13.
Pili Serikali katika Mpango wake uwe MKUKUTA au Mpango wa Miaka Mitano ya JK 2012/2016, ahaioneshi kama ina Nia dhabiti pia ya kukusanya Kodi toka kwenye kila eneo muhimu la Mapato hayo, bali limekuwa likiwaacha Wawekezaji waendelee kuchota Rasilimali yetu wakisamehewa Kodi.
Ni Ukweli usiopingika kwamba, Serikali haijakusanya Kodi vya kutosha kwenye Mahoteli yetu ya Kifahali ambayo wamepewa wawekezaji nchini wachote faidi na kuzisafirisha kwao, bado haijakusanya Kodi yoyote kwenye Bureu De Change zinazobadilisha fedha nchini na kwenye eneo la Madini.
Serikali bado haijakusanya Kodi ya kutosha kwenye Makampuni ya Simu ambayo yamekuwa yakibuni mbinu mbalimbali za kujipatia fedha, lakini kibaya wananchi ndiyo wamekuwa wakikatwa Kodi kwenye kila Uzinduzi wa Huduma za Simu, huku wao wakifaidi faida na matunda hayo na baadhi ya Vigogo.
Hapo awali Serikali iligamba kwamba, Kukatikakatika kwa Umeme katika nchi hii, ifikapo 2014/15 utakuwa historia, na ndiyo maana imeamua kujipapasa kwa sehemu kubwa kupeleka Bajeti yake kubwa kwenye Wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Fedha Fedha, Dk. William Mgimwa akifurahia na kuwatumainisha Waendesha Bodaboda, Wananchi na Wabunge kuondolewa kwa Kodi ya Vyombo hivyo, ni vizuri  wakaelewa Bodaboda na Miradi ni ya Nani! Miradi hiyo ni ya Vigogo si walalahoi hivyo ana sababu ya kurudiarudia kulisema.
Watanzania waeleweke, Pikipiki na Bodaboda zinatumia Petroli, hivyo Maumivu ya kuongezeka kwa bei  ya Mafuta iwe Dizeli au Petroli, haimuumizi mwendesha Bodaboda mwajiliwa wa Kigogo, waendeshaji ni watumwa wa vigogo, hivyo nauli kubwa itawaumizaa walalahoi wanaopanda.
Hii ina maana, Vigogo wanapunguziwa Kodi wafanye biashara kiulaini kwa gharama ndogo, lakini Mlalahoi aumie mradi faida ifike kwa Tajiri bila kujali madhara ya mwananchi wa Kawaida.
Haiingi akilini kama Serikali inaendelea kuagiza Samani za ofisini toka Ulaya, badala kutumia Samani za Rasilimali yetu ya asili ambazo ni nzuri zaidi kuliko za nje, hali hii pia inaongeza Matumizi ya Serikali pasi na Sababu.
Katika hili, Wabunge wasio na upembuzi, watadanganyika wakidhani Bajeti hii ni nzuri yenye kuwasaidia wananchi wao wakisikia bodaboda zimepunguziwa Kodi, lakini haina msaada wowote, na wananchi wanachotakiwa ni kujipanga kuangalia wabunge wenye uwezo wa kuchambua mambo yenye badala ya wale wanaoema, Ndiyoooo!.

No comments:

Post a Comment

Pages