HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 07, 2013

Mil. 16/- za MKUKUTA zahujumiwa Mvomero

Na Mwandishi Wetu, Mvomero
MILIONI 16,076, 2240/- za Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) zilizogawiwa na Halmashauri ya Mvomero kwa Kata ya Mhonda, zinawapa wehu watendaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Kiongozi mmoja akituhumiwa kuanza kuzihujumu.
Hujuma hiyo imebainika Juni 6, 2013 ambapo Wajumbe 21 wa CCM wa Halmashauri ya Kijiji cha Kichangani kilichogawiwa na Halmashauri ya Wilaya Mvomero Mil. 7,562,169/-, kutishia kujiuzulu na ikibidi kujiunga na vyama vingine, baada ya Kiongozi huyo kutoa Hundi la Mil. 2.5/-.
Mgao wa fedha hizo zinazowapa wehu watendaji hao kiasi cha CCM kukiondolea kukubarika zimegawanywa Vijiji Vitano na kiasi chake kwenye Mabano. Kichangani (Mil. 7,562,169/), Hubiri (1,332,855/-), Mafuta (Mil.1, 193,012/-), Mhonda (3,471,982/-) na Kwelukwiji (Mil.2, 516,222/-).
“Baada ya kuparangana na kutoafikiana na Hundi ya Mi.2,5/- iliyotolewa na Kiongozi wa Kata kwa Kijiji chetu cha Kichangani, alimpigia Simu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mvomero Jonas Van Zealand, na alipofika aliamuru mgao wetu tupewe kama ulivyo”.alisema mtoa habari toka ndani ya Kikao.
Tanzania Daima liliongea na wananchi na baadhi ya Viongozi wa Vijiji wa Kichangani, Hubiri, Mafuta, Mhonda na Kwelukwiji kwa nyakati tofauti, ambapo wote walielezea kutokuwa na Imani na Kiongozi huyo wa Kata Jina linahifadhiwa, kwa madai kwamba hana Uadilifu, na kwamba inasemekana amejilipa Mi. 1.5/- anazodia alikikopesha Kijiji cha Kichangani, jambo linapingwa.
“Alikikopesha Kijiji kama Nani? Nani aliyemruhusu ajilipe na kuna Makubaliano gani hadi afanye hivyo bila ya ridhaa ya sisi wananchi? Kama Mwenyekiti wa Halmashauri hatamuwajibisha au kujiuzulu mwenyewe, ambaye ameshuhudia Kosa alilofanya. Tutahamasisha kumng’oa”.Mjumbe mmoja akisema wameacha kujiuzulu sababu ya Ombi la Zealand.

Aidha hadi tunakwenda mitamboni, Zealand alipotafutwa kwenye Simu yake ya Kiganjani 0718132507 kuzungumzia tukio hilo ilikuwa imefungwa, ambapo pia Diwani wa Kata ya Mhonda Salum Mzugi 0658292149, naye hakupatikana. Ila Diwani Viti Maalum Juliana Petrol (Chadema) alisema alisafiri hivyo atalifuatilia. Na ikibainika Chama chake hakina kulala. Lakini wananchi wamesema wana Imani Zealand atalishughulikia.

No comments:

Post a Comment

Pages