Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo wakati wa hafla ya utoaji zawadi kwa washindi shindano la Twiti Wazo Jipya Kuondoa Umaskini jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Institute Of Management and Enterprenuership, Dk. Donath Olomi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi kitita cha sh. milioni 1 mshindi wa kwanza wa shindano la Twiti Wazo Jipya Kuondoa Umaskini, Jilly Gaudence Kyomo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Institute Of Management and Enterprenuership, Dk. Donath Olomi. Kulia ni mshindi wa pili, Peter George na mwanafunzi wa chuo cha CBE, Ludovick Angelino.
Mshindi wa pili, Peter George akipokea kitita cha sh. laki 5
Mshindi wa tatu akipokea kitita cha sh. laki 3.
Na Mwandishi
Wetu
VIJANA
watatu wa jijini Dar es Salaam, wameibuka washindi katika shindano la Dk.
Reginald Mengi la ‘Kutwit’ kuondoa umasikini nchini.
Mshindi wa
kwanza katika shindano hilo lililopewa jina la Twiti Wazo Jipya Kuondoa
Umasikini ni Jilly …. ambaye aliibuka na kitita cha sh milioni moja, Peter
George (sh 500,000) na Ludovick Angelino (300,000).
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika Ofisi za
Makao Makuu ya IPP, Dk. Mengi alisema shindano hilo lina lengo la kuibua mawazo
mapya jinsi ya kupambana na umasikini.
Alisema
washiriki wa shindano hilo lililozinduliwa Mei 13 na washiriki wengi
walijitokeza kuibua mawazo mapya na washiriki watatu ndio walioshinda.
Dk. Mengi
ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, alisema mchakato wa kupata
washindi, ulisimamiwa na Kiongozi wa Taasisi ya Chuo cha Uongozi na
Ujasiliamali (IMED), Donath Olomi na jopo lake.
Akizungumza
jinsi washindi hao walivyopatikana, Dk. Olomi alisema jumla ya Twits 481
zimepokelewa kati ya Mei 13 hadi 31.
Alisema
vigezo vilivyotumika katika mchakato huo ni wazo lililoeleweka na kuelezeka kirahisi, lisiwe wazo ambalo limeshasikika mara nyingi
na liwe linaweza kutekelezeka.
Alisema
mshindi wa kwanza Jilly alitoa wazo lililosema ‘Tuwe na utamaduni wa kupenda
kile tukifanyacho, tukifanya kwa moyo, uadilif, heshima na kujali muda hata
kama it’s self employed.
No comments:
Post a Comment