HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 26, 2013

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA KILOLO AFARIKI GHAFLA

 Mohamed Gwalima enzi  za uhai  wake  kulia akijiandaa kumzawadia  Kompyuta aliyekuwa katibu tawala  wa mkoa  wa Iringa Gertrude Mpaka  wakati wa hafla ya  kumuaga iliyofanyika ukumbi wa St Dominic mjini Iringa ,wa  pili  kulia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya  Kilolo Joseph Muhumba na mkuu  wa wilaya ya  Kilolo Gerald Guninita. (Picha na Francis Godwin Blog)
Mfanyabiashara maarufu mkoani Iringa na kada wa chama cha mapinduzi (CCM) Salim Abri Asas (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 3.2 kwa mkuu wa wilaya ya Kilolo Bw. Gerald Guninita  hivi karibuni ofisini kwake wanaoshuhudia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo Joseph Mhumba, kushoto na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo Momahend Gwalima ambae ni marehemu  sasa.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wilaya ya Kilolo Mohamed Gwalima. (Picha na Francis Godwin

Na  Francis Godwin, Iringa

ALIYEKUWA  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, Mohamed Gwalima afariki dunia ghafla nyumbani kwake Kilolo.

Akithibitisha kutokea kwa kifo cha Mkurugenzi huyo Mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita ambae yupo kikazi mjini Dodoma amesema kuwa mkurugenzi huyo amefariki ghafla nyumbani kwake baada ya kuwasili kutoka safari jijini Dar es Salaam usiku  wa kuamkia leo.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa alipigiwa  simu kujulishwa juu ya kifo cha mkurugenzi huyo usiku huu.

" Ni kweli ndugu mwandishi habari hizo ni za kweli kabisa nimepigiwa simu na mganga mkuu wa wilaya ya Kilolo juu ya kifo hicho"

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Joseph Muhumba alisema  kuwa kifo cha mkurugenzi huyo kimeacha pigo kubwa katika Halmashauri ya Kilolo.

Kwani alisema kabla ya kifo cha ghafla cha mkurugenzi huyo alikuwa nae jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutafuta wahisani wa kusaidia kufufua kiwanda cha Chai kidabaga ili kuwakomboa wananchi wa wilaya hiyo.

Alisema kuwa mbali ya kuwa kifo hicho kimetokea ghafla ila mkurugenzi huyo kabla ya kifo chake alikuwa akilalamika kusumbuliwa na tatizo la Kisukari .

Muhumba alisema kuwa kifo cha mkurugenzi huyo kilitokea ghafla usiku wa kuamkia leo baada ya kurejea kutoka jijini Dar es Salaam ,pia amewapa pore nyingi wananchi wa Kilolo kwa msiba huo mzito.
Wakati  huo  huo waombolezaji   walifika kuaga mwili wa mkurugenzi huyo walieleza kusikitishwa kwao na hatua ya kamati ya mazishi kushindwa kutoa nafasi kwa watumishi wa Halmashauri ya Kilolo na Halmashauri nyingine mkoa wa Iringa pamoja na wananchi kuaga mwili huo.
Mbali ya waombolezaji hao zaidi ya 500 kufika mapema zaidi katika viwanja vya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa ajili ya kuaga mwili huo ila hali imekuwa tofauti baada ya kuwepo kwa ratiba zinazochanganya zaidi ya mbili.

Taarifa za awali zilizotolewa zilionyesha kuwa mwili huo ungeagwa majira ya saa 4 asubuhi ila baadhi ya watu waliofika mida hiyo kuaga waliambiwa kuwa mwili huo ungeagwa mida ya saa 7 mchana na baada ya kufika majira ya saa 7 mchana lilitolewa tangazo jingine na kaimu mkurugenzi kuwa taratibu za kuuandaa mwili zinaendelea na mara baada ya kuaga basi mwili huo utapelekwa msikitini .
Hata hivyo hali haikuwa hivyo wananchi waliokuwa wamejiandaa kwa ajili ya kuaga mwili huo walijikuta wakiduwaa baada ya mwili huo kutolewa chumba cha maiti na kupakiwa katika gari kisha kupelekwa msikitini na baada ya msikitini mwili huo uliingizwa katika gari jingine la wagonjwa na kuondoka kuelekea kijiji cha Ikwiriri Rufiji kwa mazishi yatakayo fanyika kesho.

Baadhi ya watumishi waliofika kuaga mwili huo wameonyesha kusikitishwa na hatua ya kutouaga mwili wa mkurugenzi wao,
marehemu alizaliwa tarehe 16 februari 1957 ikwiriri rufiji na kupata elimu ya sekondari kidato cha kwanza mpaka kidato cha nne katika shule ya sekondari same kuanzia mwaka 1978-1980 alipata elimu ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari shinyanga
mwaka 1980 mpaka 1981 alitumikia taifa katika jeshi la kujenga taifa kabla ya kujiunga na masomo ya shahada ya uchumi katika chuo kikuu cha dar es salaam,stashahada aliyotunukiwa mwaka 1986
Mara baada ya kutunukiwa shahada ya uchum i mwaka 1986,aliajiriwa kama mchumi katika halimashauri ya wilaya ya Mtwara.
Al;itumikia taifa katika maeneo mbalimbali kama mchumi mpaka mwaka 2007 alipoteuliwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Mbulu.

Mwaka 2012 alihamishiwa katika halimashauri ya wilaya ya Mtwara na mwaka huu 2013 alihamishiwa katika halimashauri ya wilaya ya kilolo ambako amekuwa mkurugenzi mtendaji wa halimashauri hiyo mpaka mauti ilipo mfika tarehe 25/06/2013 saa 1:15 jioni katika nyumba aliyokuwa anaishi na familia yake ilyopo karibu na ofisi za halimashauri hiyo.

MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA

No comments:

Post a Comment

Pages