HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 19, 2013

PPF IKATAE MCHEZO MCHAFU WA WAAJIRI


Mkurugenzi Mkuu wa PPF,  William Erio
Na Bryceson Mathias

MFUKO wa Pensheni ya Mashirika ya Umma (PPF) na Waajiri nchini, wametakiwa kuacha siasa na Mchezo Mchafu wa kutotekeleza Sheria za nchi na kukalia Mafao ya wafanyakazi na wastaafu waliojiandikisha na Mfuko huo, na baadaye kurithi tabu na familia wakistaafu.

Inasikitisha kuona, PPF kwa muda mrefu imekuwa chanzo cha kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria Waajiri wasiopeleka Michango ya asilimia 5% Walizokatwa wafanyakazi kwenye mishahara, na Mchango wa Mwajiri wa 15% kutimiza 20% ya Mkataba.

Pamoja na PPF kujigamba imekuwa iko mstari wa mbele kutoa huduma nzuri kwa wananchama wake, lakini Mfuko huo kupitia kwa baadhi ya maofisa ulijichafua Dhidi ya Dhuluma za makato hayo kwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukarii Mtibwa kutofishwa PPF.

Kimsingi, nina ushahidi wa PPF jinsi ilivyozikanyaga Sheria zake yenyewe ilizoridhia kisheria, iwapo mwajiri atashindwa kuwasilisha michango ya Mteja kwa muda ulioainishwa kisheria. Wateja wengi wa Sukari Mtibwa Michango yao nay a Mwajiri haikufikishwa PPF hadi kushitakiana na Mwajiri akaadhibiwa!

Mwajiri aliadhibiwa awalipe wadai kwa kucheleweshewa kufikishwa michango yao PPF Shilingi Laki 500,000/-kwa kila Mteja, aliyewasilisha dai lake, lakini waliokuwa kazini walishindwa kuanika madai yao kwa hofu ya kufukuzwa ajira zao.

Wafanyakazi takribani zaidi ya 1000, wamefariki katika Kiwanda hapo (Orodha ninayo) huku wakiwa hawajanufaika na Ustaafu wao na wengine kuacha familia zao zikikosa masomo ya kuwasaidia katika maisha yao kwa sababu asilimia 5%+15%=20% hazikufika PPF.
Kuhodhiwa kwa Makato hayo na Mwajiri, ni kosa la Jinai Kisheria, maana licha ya kumvurugia Mstaafu au Mwajiriwa Maisha na Mtiririko na Mpango mkakati wa Dira ya Maisha yake, lakini unajenga Uhasama na Uadui miongoni mwa watendaji wenye dhamana na raia.

Uwekezaji wa Mtibwa ambao umefanywa na Wazawa miongoni mwa wabia wakituhumiwa kuwemo waliokuwa Vigogo wa Serikali wakiwemo Wabunge maarufu, ni Aibu na Doa kubwa kwa Jamii, hasa ukizingatia Vitukuu, Wajukuu na Watoto ni wazawa wa eneo hilo wanaotazamana.

Hata kama Wabia au Vigogo hao watakuwa na Heshima za Kitaifa na Kimataifa ndani na Nje ya Nchi katika Kada mbalimbali, lakini inapofika wanamuona Kiongozi huyo anatoa misaada kwa walemu au watu wasiojiweza sehemu kadhaa wakati ameadhulumu haki sehemu hiyo; Heshima yake inaporomoka!

Tabia hizo, ndizo zilizosababisha Serikali na Chama Tawala (CCM), kipoteza Umaarufu wake katika maeneo mengi ilikopoteza Utawala wake wa kiadlifu, na kuwapa mtaji washindani, kutokana dhambi za wazi ambazo vizazi hivyo vimefanyiwa na kuwa Donda Ndugu.
Hata naandika Makala hii, wastaafu na Wafaanyakazi hawajalipwa Masurufu hayo, na kibaya zaidi bila huruma wala aibu Vizazi vilivyokanyagwa haki zao vipo, na wastaafu wanasota na haki hizo wapo, PPF ikijinadi na Ubora!

Kama Mwandishi hadi nahojiana na aliyekuwa Meneja wa PPF Kanda ya Kati Morogoro Meshack Bandawe ambaye sasa alihamishwa na kuwa Meneja wa Kanda ya Ziwa, bado wanfanyakazi waliopunguzwa kazi katika Kiwanda hicho, Michango yao hiyo ilikuwa bado ni tete.

Ni rai yangu Katika Ushindani huu wa Mifuko ya Pensheni, PPF inatakiwa kujitathmini, ili makosa ya Nyuma yasifishwe yasiendelee kuwawekea Kovu na Haki ya Wastaafu wa Mtibwa wapewe, badala ya kudhulumu na kupata Laana za Vizazi dhidi ya viongozi wao wa Kitaifa.

nyeregete@yahoo.co.uk 0754-933308

No comments:

Post a Comment

Pages