Na Elizabeth John
WAREMBO wanao
wania taji la Redds Miss Kinondoni 2013/2014, leo wamefanya usafi katika hospitali ya Mwananyamala pamoja na kujionea hali
ilivyo mbaya kwa wagonjwa.
Akizungumza baada
ya kumaliza usafi huo, Redd’s Miss Kinondoni ambaye pia ni Miss Tanzania,
Bridget Alfred alisema wameamua kufanya hivyo wakiwa na lengo la kufanya
harambee ya kuchangisha hela kwa ajili ya kununua vitanda kwa akina mama
wanaojifungua.
Alisema harambee
hiyo itafanyika keshokutwa katika ukumbi
wa Ambassador Lounge uliopo Posta jijini Dar es Salaaam na Meya wa Manispaa ya
Kinondoni, Yusuf Mwenda anatarajia kuwa mgeni rasmi.
“Huu ni mwanzo
tub ado tunaendelea kutembelea hospitali mbalimbali, leo tumeanza Mwananyamala
kesho (leo) tutakua hospitali ya Sinza pamoja na kutembelea mradi wa mabasi
yaendao kasi,” alisema mrembo huyo.
Mashindano hayo
ya Redds Miss Kinondoni yanatarajiwa kufanyika Juni 21 mwaka huu na
yamedhaminiwa na Redds Orijino, Chilly willy energy drink, Oriflame natural
beauty products, Times Fm na Jb Belmont hotel.
Naye Mganga Mkuu
wa Manispaa ya Kinondoni, Dk Gunin Kamba aliwashukuru waandaaji wa mashindano
hayo kwa harambee hiyo ambayo itasaidia afya za wagonjwa wa hospitali hizo kwa
kiasi fulani.
“Mimi naomba
wananchi wengine waige mfano huo kwani jukumu la usafi ni la kila mtu sio
kuisubiri serikali peke yake, naomba liwe zoezi endelevu lisiishie hapa,”
alisema Dk Kamba.
No comments:
Post a Comment