Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2013, akifafanua jambo wsakati wa uzinduzi wa shindano hilo. (Picha zote Habari Mseto Blog)
Mshindi wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012, Walter Chilambo akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012, Walter Chilambo (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa BenchMark Production Rita Poulsen na Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan.
Mkurugenzi Mtendaji wa BenchMark Production Rita Poulsen akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa shindano la Epiq Bongo Star Search jijini Dar es Salaam leo.
DAR ES SALAAM, Tanzania
SHINDANO la
Epiq Bongo Star Search linatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 29 mwaka huu huku
likiwashilikisha wadau wakubwa wa muziki hapa nchini kwa lengo la kuwajenga
washiriki kwa kuwapa ujuzi zaidi utakaowasaidia kukua kimuziki.
Akizungumza
katika makao makuu ya Kampuni ya simu za Mkononi ya Zantel ambao ni wadhamini
wakuu wa shindano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa BenchMark Production Rita
Poulsen alisema, shindano hilo linatarajiwa kufanyika usajili katika Mikoa Sita
ambayo ni Mwanza, Mbeya, Arusha, Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam.
Rita alisema,
Mwaka huu kauli mbiu ‘Kamua’ na kudai kuwa wamejipanga kuwafikia vijana wengi
hapa nchini, na pia kutengeneza nyota wengi wa muziki mbali na mshindi na kudai
kuwa wataanzia Mkoani Dodoma Juni 29-30, katika ukumbi wa Maisha klabu, Julai
5-6 Zanziba Hotel ya Bwawani, Mbeya Julai 10-11 Klabu Vybes, Mwanza Julai 14-15
Klabu Fassion, Arusha Julai 20-21 Tripple A na kumalizia Dar es Salaam Julai
26-28 uwanja wa Taifa.
Naye Ofisa
Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema, Zantel wanajivunia kufanya kitu
kikubwa kama hiki ambacho kinawapatia vijana ajila, na kudai kuwa, wanatarajia
kufungua laini ya kurekodi kwa simu kuanzia siku ya kwanza ya usaili Mikoani
ambapo washiriki watapiga namba 0901551000 au kutuma neno Kamua kwenda 15530.
Epiq BSS,
imekuwa ikiwatoa vijana katika hali ya umasiki na kuwapa ajili kama ilivyo kwa
wasanii kama Kala Jeremaya ambaye anatikisa katika muziki wa Hiphop pamoja na
Walter Chilambo aliyetwaa taji hilo mwaka jana.
No comments:
Post a Comment