HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 26, 2013

SHUKRANI

MARIETHA NJIMBA (MRS. MZEE MFAUME)
Familia ya MZEE MFAUME na Wazazi Bw & Bibi CLAUDE NJIMBA wa Kinyerezi na Tabata Dar es salaam wanapenda kutoa Shukrani kwa wote walioshiriki  katika msiba wa mpendwa wao MARIETHA NJIMBA (MRS. MFAUME) kilichotokea tarehe 29/05/2013 na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni tarehe 01/06/2013.

Shukrani za pekee tunazipeleka kwa Uongozi na wafanyakazi wote wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Kisanga, Dk. Mary, wauguzi wa Burhan Hospital, Mapadre na Waumini wa Parokia Katoliki ya Kinyerezi, Kristu Mfalme–Tabata, Majirani, Ndugu,  Jamaa na Marafiki wote kwa jinsi mlivyoshirikiana nasi katika msiba huo. Sio rahisi kuwataja kwa majina wote walioshiriki nasi. Tunaomba mzipokee shukrani zetu kwa waraka huu.

Shukrani za kumaliza msiba huo zitafanyika nyumbani kwake Kinyerezi, siku ya Jumamosi tarehe 06/07/2013 kuanzia 02 asubuhi kwa Ibada ya Misa Takatifu nyumbani kwa Marehemu. Tunawakalibisha wote.

              BWANA  AMETOA  NA BWANA  AMETWAA  JINA  LAKE  LIHIMIDIWE.

No comments:

Post a Comment

Pages