HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 20, 2013

‘SIPENDI KUIONA SOWETO YA TANZANIA'

Na Bryceson Mathias
WAKATI wananchi wa Afrika Kusini chini Mpigania Uhuru, Nelson Mandela, walipokuwa wakidai Uhuru wa kujikomboa, ilifikia mahali kule Soweto, Askari wa Makaburu waliwaua watu waliokuwa wakisonga mbele wakitaka ukombozi, baadaye wakalewa Damu na kuacha!.
Naonya Sipendi kuiona Hali hiyo ikijiri Tanzania, tukawa na Soweto ya Pili Afrika, mbali ya ile iliyoleta ukombozi wa kilio ambao hautasahaulika vizazi na vizazi vya Historia ya Afrika dhidi ya Makaburu chini ya Shujaa na Kiongozi aliyewekwa Mungu; Mandela.
Nilikuwa nabubujikwa Machozi, nikiona Waumini Makanisa, Misikiti na Familia Binafsi za Afrika Kusini, kwa pamoja wanavyomuombea Rais Mstaafu, Nelson Mandela, ambaye anatibiwa homa ya mapafu, pneumonia.
Taarifa zinasemaJumamosi msemaji wa Rais, Mac Maharaj, alieleza kuwa Bwana Mandela aliweza kuvuta pumzi bila ya shida na alipata nafuu, lakini bado wasi-wasi uliokuwa ungaliko kuhusu kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 94, uliwapa moyo wa kuomuombea!
Mandela aliishi mtaa wa Soweto, Johanneburg, kwa miaka mingi. Mkaazi mmoja wa Soweto, Eddie Vilakazi, aliyemuombea Mandela katika ibada ya Jumapili, akiongea alisema,
“Natumai mzee huyu ataishi muda mrefu. Mandela ni kiongozi wetu, Tunamuona kuwa mkombozi wetu..., Mandera ni kila kitu kwetu..., Tunamtakia afya njema haraka, Mungu amuangalie, ambariki kwa sababu tayari ameshabarikiwa..Lakini tunamtakia maisha marefu zaidi, awe nasi”.alisema!
Upendo ule niliouona, na Mavazi Meupe ya Amani ambayo watu walikuwa wamevaa nyakati zote za kumuombea kila mahali walipo, yaliniliza machozi; nikakumbuka Kilio tulichotoa baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipotutoka, nikilinganisha na hali tuliyonayo sasa nchini!
Najiuliza! Je, Watanzania tutafikia upendo wa kupendana kama ule wanaonesha Wa-Afrika kusini dhidi ya Baba yao wa Ukombozi Mandela? Kama sisi wenyewe tunaweza kunyofoana kucha, kutoana Meno, kutoboana Macho, kumwagiana Tindikali na kumwagiana Damu?
Hali tunayokwenda nayo, tutapofushana Macho wenyewe, tutapeana Ulemavu wenyewe, Tutauana wenyewe, na kupeana Majeraha wenyewe, wenye raha na furaha ya mambo hayo, watakuwa Ulaya!!! Sisi tukiumizana. Wakija watatusanifu na kutuona wakuja, kumbe nchi hii ni yetu sote.
Kama makaburu waliwaua Wa-Afrika hadi wakaona hii siyo sahihi, kwa nini sisi weusi kwa wausi tusiwe na uchungu zaidi ya Makaburu? Ni kweli Ng’ombe wa Maskini hazai au Kuokota na akiokota huambiwa Kaiba!. Je uhuru wetu huu tumeuiba? Tujue
Nyerere aliufanyia kazi.
Imefika mahali sasa watu hapa nchini watakuwa vipofu wa kusababishia wenyewe kwa wenyewe; Kwa sababu ya Moshi wa Mabomu ya Machozi na Maji ya kuwasha! Kama tunawalaumu na kuwachukulia wawekezji wanaoharibu Mazingira kwa kutiririsha Maji Machafu, lini tutaona Mabomu ya Machozi na Maji ya kuwasha yanaharibu Mazingira?
Nimeshangaa kuona Tanzania sasa, wananchi wakisikia Mabomu ya Machozi yanapigwa na Askari, wanashangilia, kwa maana ya kwamba Ubungo umezoe, akili imezoea, mwili haushituki, Polisi wanamuona ni Babu au Bibi, na inapofika hapo hali ni mbaya tutafikia ya Soweto!
Watawala; Nani anapenda hali hiyo? Viongozi wa Dini; Nani anapenda hali hiyo ikithiri? Wana-harakati, nani anaridhia hali hii ishamiri? Hivi kama ya Arusha angefanyiwa hivyo, Baba yako, Mama, Mke wako, Mwanao, Mjomba, Shangazi nk. Ungefurahi na kutoa kebehi? Msiba ni Mzuri ukiwa kwa Jirani!
Sipendi kuiona ‘Soweto ya Tanzania’, nataka kuombeana kama kwa Afrika kusini! Wanavyomuombea Mandera
nyeregete@yahoo,co.uk 0715-933308

No comments:

Post a Comment

Pages