Na Elizabeth John
WIMBO unaokwenda kwa jina la ‘Tupo
Wangapi’ ulioimbwa na wakali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Suma Mnazareti
na Tunda Man unafanya vizuri katika tasnia ya muziki huo kutokana na ujumbe
uliobeba.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Suma alisema wakati anatunga mashairi ya wimbo huo, waliangalia hali halisi
ya mapenzi ya wakinadada wa Kitanzania ambayo kila siku yanakua na sura mpya.
“Unajua kila msanii ana mashabiki
wake hivyo naamini kutokana na kufanya kazi na Tunda kumenisababishia kuzoa
mashabiki wengi ikiwa ni pamoja na kusimama kwa mashairi yake,” alisema Suma
Mnazareti.
“Nashukuru kazi zangu zinapokelewa
vizuri na mashabiki, kitu ambacho kinaniongezea uwezo wa kuendelea kuandaa kazi
nyingi ili kuendelea kufurahisha jamii pamoja na kuielimisha kupitia fani hii,”
alisema.
Alisema amekuwa akiumiza kichwa
kila siku kwa ajili ya kutengeneza vitu vizuri vyenye ujumbe kwa jamii, lengo
lake likiwa ni kutoka kimaisha kupitia muziki.
No comments:
Post a Comment