Na Elizabeth John
SHIRIKISHO la
ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) linatarajia kufanya uchaguzi wake Mkuu Julai 7
mwaka huu jijini Mwanza baada ya viongozi waliopo madarakani kumaliza muda
wake.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga, alisema nafasi
ambazo zitagombewa ni Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu, Mweka Hazina na
nafasi tisa za wajumbe.
Mashaga alisema fomu
zilianza kutolewa Juni 4 katika Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa
(BMT)na kwamba usaili kwa wagombea wote utafanyika Julai 5 jijini Mwanza.
Alisema gharama za
fomu hizo kwa wagombea ni sh. 150,000 nafasi ya Rais, sh. 100,000 kwa nafasi
ya Makamu wa Rais, Katibu Mkuu na Mweka Hazina, sh. 50,000 kwa wajumbe.
Aliongeza kuwa Shirikisho
linatoa wito kwa watanzania wenye uwezo wa kuongoza michezo kujitokeza kwa
wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi hizo kwa miaka mine ijayo.
No comments:
Post a Comment