HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 06, 2013

MASHINDANO YA RIADHA YA TAIFA YAPIGWA KALENDA

Na Mwandishi Wetu

BAADA ya Zanzibar kujitoa kuwa mwenyeji wa mashindano ya vijana ya riadha ya kanda ‘Eastern Regional Jr Championship’ hatimaye mashindano hayo yamepigwa kalenda hadi Juni 13 mwaka huu ambapo yatafanyika jijini Dar es Salaam.

Tanzania ilikuwa imepewa uenyeji wa mashindano hayo, ambapo Chama cha Riadha Tanzania (RT), kikaipa Zanzibar; mashindani ambayo yalikuwa yafanyike Juni 8 na 9 kwenye Uwanja wa Amani, lakini kwa sasa yatafanyika katika Uwanja wa Taifa jijini humo.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa RT, Mujaya Suleiman Nyambui, alisema mashindano hayo yatakayoshirikisha nchi 10 yamesogezwa mbele kutokana na mabadiriko hayo yaliyojitokeza.

“Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na tunaamini maandalizi yataenda vizuri ili mashindano yafanyike kama yalivyo pangwa” alisema Nyambui.

Alisema nchi zitakazoshiriki mashindano hayo ni Kenya, Uganda, Somalia, Misri, Eritrea, Ethiopia, Djibouti, Sudan, Zanzibar na wenyeji Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages