Na Mwandishi Wetu
WAKAZI wa Kata ya Saranga
wameutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam,
kusambaza makasha ya kutupia taka, lengo ni kuifanya kata hiyo kuwa na
mazingira bora wakati wote.
Akizungumza na wandishi
wa habari jijini, Katibu wa BAVICHA, kata hiyo, Lazaro Lucas, alisema
kujitokeza kwa wananchi wengi vile bila kujali itikadi ya vyama inadhihirisha
kuwa wamechoshwa kuishi kwenye mazingira machafu.
Alisema kusambazwa kwa
makasha mengi ya kutupia taka kutawafanya wakazi wa kata hiyo kujizuia kutupa
taka hovyo kwenye mitaa.
“Leo mkusanyiko wetu huu
tumeamua kufanya usafi kwenye mtaa huu wa Matangini lakini huu ni mpango
endelevu, utaendelea kufanyika kwenye mitaa yote saba ya kata hii kwa
ushirikiano kama huu”alisema Lucas.
Alisema utaona baadhi ya
watu wamepiga pasi nguo zao vizuri lakini cha kushangaza watu hao wamezunguukwa
na uchafu katika makazi na ofisi zao
kitendo kinachowashushia hadhi.
“Huwezi kuwa umenyoosha
nguo zako vizuri kwa pasi lakini unaishi na uchafu itakuwa usafi wako wa nguo
ni bure tu, bado utakuwa wewe ni mchafu”alisema.
Naye Diwani wa kata hiyo,
Efraim Kinyafu, alisema suala la usafi na utunzaji wa mazingira ni mpango
mkakati wa wilaya hiyo, ambao unamhusu kila mtu.
Alisema ni lazima kwa
wakazi wa saranga na kwa ujumla kuwa wanahakikisha wanaweka kata hiyo katika
mandhari safi nay a kuvutia wakati wote.
No comments:
Post a Comment