HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 24, 2013

WATANO WASHITAKIWA KWA UGAIDI TABORA

Ni viongozi na wafuasi wa Chadema
 
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar es Salaam na vijana wengine leo wameshtakiwa kwa Ugaidi katika mahakama ya Hakimu mkazi Tabora mjini.

Mbali ya Kileo, vijana wengine wa Chadema, ni  Evodius Justinian wa Buboka, Oscar Kaijage wa Shinyanga, Seif Magesa Kabuta wa Mwanza, Rajab Daniel Kihawa wa Dodoma, leo wamesomewa shitaka la Ugaidi kwa kumteka na kumwagia tindikali Musa Tesha katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa Igunga uliofanyika mwaka 2011.
Watuhumiwa hao walisomewa mashtaka mawili wote, la kwanza ni la kufanya ugaidi, na la pilini kumwagia tindikali Musa Tesha.

Kesi hiyo ilikuwa ilisikilizwa mbele ya hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, ya Tabora Mjini,Joktani Rushwera, huku upande wa serikali ukiwakilishwa na Wakili Juma Massanja na Ildefons Mukandara Baada ya kusomewa shitaka hilo, Upande wa utetezi wa ukiongozwa na wakili Prof Abdalah Safari, ukiwajumlisha Peter Kibatala na Gasper Mwalyela ulitoa hoja kuiomba mahakama hiyo ifutilie mbali mashtaka hayo kwa sababu, kwanza mashtaka hayakuwa na uhai kwa kuwa yamefunguliwa bila ridhaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini. 

Sheria za uendeshaji wa makosa kama hayo hapa nchini zinadai kuwa mashataka kama hayo yanapofunguliwa ni lazima ridhaa ya Mkurugenzi wa mashtaka iwepo. Kwa kuwa ridhaa hiyo haikuwepo, mawakili waliiomba mawakili kuitupilia mbali kesi hiyo.

Sababu ya pili iliyotolewa na upande wa Utetezi ilikuwa kwamba maelezo ya kesi kuwa ni ya ugaidi, yalikuwa hayaonyeshi kuwa ni ya kigaidi tofauti na makosa mengine ya kawaida kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, hivyo waliiomba Mahakama kutupilia mbali shitaka hilo au lifunguliwe kama kosa la kawaida.

Na sababu ya tatu ilikuwa ni kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai, sheria inaelekeza kuwa mshitakiwa ashitakiwe katika mahakama yenye mamlaka na hadhi kama ile waliyopelekwa katika maeneo yale walikokamatwa. Hivyo mawakili waliiomba mahakama itupilie mbali shitaka, kwani washitakiwa kama walikuwa na hatia walipaswa kushitakiwa katika maeneo yao walipokamatwa. Baada ya hoja hizo, Mahakama iliahirisha kesi hiyo na itatajwa tena  Julai 8 mwaka huu Tabora Mjini.

Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi au wafuasi wa chadema kufunguliwa kesi zinazohusiana na ugaidi, tarehe 18 Machi 2013, Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Wilfred Lwakatare, la Ludovick Joseph  walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka manne yakiwemo ya ugaidi.

Kosa jingine lililowakambili Lwakatare na Ludovick  ni kula njama; kosa ambalo pia linawakabili washtakiwa wote ambalo ni kinyume na kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002.
Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka Msaki  kinyume na kifungu  cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.

Katika kosa la tatu, washtakiwa wote wawili wanadaiwa kufanya mkutano wa kupanga kufanya makosa ya ugaidi  kinyume na kifungu cha 59(a) cha Sheria ya Kuzuia ugaidi.

Wakili wa serikali alidi kuwa washitakiwa wote  Desemba 28 Mwaka jana walishiriki katika mkutano wa kupanga kufanya vitendo vya kumteka nyara Msaki  kinyume na kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia ugaidi.

Pamoja na tuhuma hizo, 8 Mei, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilimfutia mashitaka matatu ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare.

Katika uamuzi huo Jaji Lawrance Kaduri akitoa uamuzi huo  alisema ulitokana kukubaliana na hoja ya  mawakili wa Lwakatare; Tundu Lissu, Peter Kibatara na Mabere Marando na kusema kuwa.
“Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, mahakama inatoa amri ya kumfutia Lwakatare mashitaka matatu, yaani kosa la pili, tatu na la nne kwa sababu Jamhuri imeshindwa kuonesha maelezo yanayotesheleza kumshitaki Lwakatare kwa kesi ya ugaidi.

“Naamuru jalada la kesi ya msingi lilirudishwe Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya mshitakiwa kuendelea kushitakiwa kwa kosa moja la kula njama ambalo linaangukia katika sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002,” alisema Jaji Kaduri

No comments:

Post a Comment

Pages