Askari wa Manispaa ya Ilala
wakiendesha zoezi la kuondoa wafanyabiashara ndogondogo katika eneo Posta mpya
jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni operesheni ya kusafisha jiji la Dar es
Salaam kabla ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama. (Picha na Habari Mseto Blog)
Vifaa vya wafanyabiashara vikichuliwa na askari wa jiji leo.
DAR ES SALAAM, Tanzania
DAR ES SALAAM, Tanzania
HALMASHAURI ya Wilaya ya
Ilala, imesema operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo kwenye maeneo
ambayo si rasmi itakuwa endelevu, imewataka wanafanyabiashara
hao kuondoka mara moja kinyume chake
wataondaondolewa kwa nguvu.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo, msemaji wa Halmashuri hiyo, Tabu Shaibu,
alisema operesheni hiyo ni mkakati wa viongozi wa halmashauri hiyo katika hali
ya usafi.
Alisema operesheni hiyo itaendeshwa
katika kila eneo la wilaya hiyo, itawahusu wale wote wanaofanyabiashara kinyume
cha sheria za halmashauri hiyo ambapo wale waliofuata utaratibu haitawagusa.
“Ujio wa Obama unaweza ukawa
sababu lakini lazima tukubali kuwa katika mila zetu majumbani kwetu tumekuwa na
ustarabu anapokuja mgeni huwa tunajaribu kuyaweka mazingira yetu kwenye
usafi”alisema Tabu. Tabu alisema operesheni hiyo katika Mtaa wa Kivukoni iliaza
jana kutokana na ukweli kwamba huko ndiko kwenye Ikulu ya Rais na viongozi
wengine wa Serikali.
Kuhusu polisi kushiriki kwenye
operesheni hiyo, alisema uamuzi huo ulitokana na viongozi wa Mkoa huo,
hata hivyo lengo ni kushirikisha kila
mdau wa wilaya hiyo, hivyo si ajabu kuona polisi wanafanya hivyo.
Aidha, wafanyabiashara hao
walitakiwa kujaribu kujiunga kwenye vikundi na kuomba maeneo ya kufanyia
biashara kisheria kupitia viongozi wa Mitaa, Kata hadi kwa Mkurugezi.
No comments:
Post a Comment