Na
Elizabeth John
BAADA ya kufanya vizuri na ngoma
yake ya ‘Naenda Kusema kwa mama’, Kinda wa muziki wa kizazi kipya nchini, Asilahi Isihaka Dogo
Asley, amefunguka juu ya uhalisia wa wimbo wake mpya wa ‘Bado Mdogo’,
liomshirikisha mwanadada Estelina Sanga ‘Lina’.
Wimbo huo ambao unazungumzia mama
anaependa kufatilia watoto wadogo na kuwataka kimapenzi, tayari umeanza kufanya
vizuri katika vituo mbalimbali vya redio kutokana na ubora wa mashairi yake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Dogo Aslay alisema wimbo huo ni kwa ajili ya kuwaelimisha vijana juu ya
maswaha hayo, lakini pia ni story ya kweli iliyomtokea yeye akiwa na miaka 16
pale tu alipotoka na ngoma yake ya kwanza ‘Naenda kusema kwa Mama’.
“Mimi nataka tu kuwaambia vijana
wenzangu kwamba usiombe yakukute mambo haya wewe yasikie tu kwa watu, huo wimbo
ni historia ya kweli na ukimuangalia mama mwenyewe hata mama yangu mzazi
hamkuti kiumri,” alisema.
Pia aliwataka wapenzi wa kazi zake
kumpa sapoti katika kazi zake zilizopita pamoja na zinazo kuja na kwamba wakae
mkao wa kula kwaajili ya kuipokea video ya ngoma hiyo ambayo inafanya vizuri
katika chati ya muziki huo.
No comments:
Post a Comment