HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 13, 2013

Huduma za masikio kwa wakazi wa Dar es salaam na watoto zatolewa

 Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing  William Austin akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam juu ya huduma ya vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo wanatarajia kuitoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.
 Baadhi ya wakazi na watoto kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam wakiwa katika foleni ya kupatiwa matibabu ya huduma ya vifaa vya kuwasaidia kusikia kutoka Mfuko wa Starkey Hearing  leo jijini Dar es salaam. Mfuko   huo umeweka kambi katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambapo wanatarajia kutoa huduma hiyo bure kwa watu zaidi ya 2000 kwa kipindi cha nne.
 Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing  William Austin (kulia) akisaidiana na Mkewe  Tani Austin(kushoto) kumuvalisha kifaa cha kumwezesha kusikia mtoto  Lilian Vincent (leo) jijini Dar es salaam wakati Mfuko huo ulipoendesha huduma ya kutoa  vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo wanatarajia kuitoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena. 
 Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing  William Austin (kulia) akisaidiana na Mkewe  Tani Austin(kushoto) kumuvalisha kifaa cha kumwezesha kusikia mtoto  Malechela Juma (katikati) leo jijini Dar es salaam wakati Mfuko huo ulipoendesha huduma ya kutoa  vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo wanatarajia kuitoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.
 Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing  William Austin (wa tatu kutoka kulia) akiwa amemkumbatia Mkewe  Tani Austin leo jijini Dar es salaanm katika picha ya pamoja na Teddy Mapunda (wa pili kutoka kulia) wakati wa zoezi la utoaji wa vifaa  vya kuwasaidia kusikia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia wa jiji la Dar es salaam ambayo itatolewa kwa wakazi zaidi ya 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hoteli ya Serena wakishirikiana na wafanyakazi wa  Mfuko wa Starkey Hearing  kuwavisha vifaa cha kuwawezesha kusikia wakazi mbalimbali wa jijini Dar es salaam leo wakati Mfuko huo ulipoendesha huduma ya kutoa  vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo wanatarajia kuitoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne.

No comments:

Post a Comment

Pages