HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 17, 2013

MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO ABUJA NIGERIA, AONDOKA LEO KUREJEA TANZANIA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Watanzania waishio mjini Abuja, wakati alipokutana nao katika Makazi ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Nigeria, jana Julai 16, 2013 na kufanya nao mazungumzo. Makamu ameondoka leo mjini Abuja kurejea nchini Tanzania, baada ya kuhudhuria Mkutano wa 12 wa siku mbili wa Afrika uliokuwa ukijadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, Julai 15-16, 2013 mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika. Kushoto kwake ni mkewe, Mama Asha Bilal. Picha na OMR 
 Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, aliyemaliza muda wake, Siwajibu Baraka Siwajibu, akiwatambulisha baadhi ya Watanzania kwa makamu wa Rais, wakati alipofika kuzungumza nao katika Makazi ya Balozi wa Tanzania, Abuja Nigeria jana Julai 16, 2013. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal, na kutoka (Kulia) ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Seif Rashid, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Mahadhi na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Fatma Rajabu. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment

Pages