JESHI
LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
11
Julai, 2013
Taarifa
kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linaadhimisha siku ya mashujaa kila tarehe 25
Julai, ikiwa ni sehemu ya kuwakumbuka mashujaa
waliopigana na kushinda vita ya Kagera mwaka 1978/1979.
Maadhimisho hayo hufanyika mara moja kwa mwaka, na mwaka huu
yatafanyika tarehe 25 Julai 2013 katika mkoa wa Kagera wilaya ya Bukoba kwenye
makaburi ya mashujaa yaliyopo Kaboya.
Mgeni rasmi katika
maadhimisho hayo atakuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri
Jeshi Mkuu Dkt. JAKAYA MRISHO KIKWETE.
Sambamba na mgeni
rasmi, watakuwepo viongozi waandamizi wa Serikali, vyombo vya Ulinzi na Usalama,
vyama vya siasa, taasisi za dini na taasisi mbalimbali za kiraia.
Vyombo
vya habari vinaalikwa kushiriki katika maadhimisho hayo ambayo
ni muhimu kwa Taifa.
Imetolewa
na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao
Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP
9203, Simu: 0764742161
Email:
ulinzimagazine@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment