HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 12, 2013

VIONGOZI MOROGORO WATAKIWA KUDHIBITI MIFUGO

Na Bryceson Mathias, Mvomero
 
MWENYEKITI wa CHADEMA Kata ya Sungaji Wilaya ya Mvomero, Musa Kombo, amesema Viongozi wa Mkoa na Wilaya akiwemo Mbunge wao Amosi Makalla, wanaoshindwa kuwadhibiti wafugaji na kuwaacha waharibu Mazao ya wakulima na kuwasababishia Njaa; Wawajibike!
 
Kombo alitoa Kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa Mkutano uliofanywa Kijiji cha Kigugu 11.7.13 saa 7-10 jioni na Naibu Waziri wa Habari, Michezo Vijana na Utamaduni, Amos Makala, alipojibu Ki-Wepesi Maswali manne Magumu, yaliyoulizwa na  Wananchi hao.
 
Akimjibu Makalla Kombo alisema, Imefika mahali Viongozi wa Mkoa na Wilaya akiwemo Mbunge, wanapaswa kuwajibika kutokana na kushindwa kuwathibiti Wafugaji wanaoharibu mazao ya wakulima waliyolima ili wajikimu njaa na kuuza wawasomesha watoto, hali iliyoonesha Waziri ametofautiana na Wananchi kimsimamo walivyotarajia aseme.
 
Alidai, “Makalla Kusema, hata Mimi ni kama ninyi, na kwamba Suala la Wafugaji ni gumu hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameshindwa kutoa Suluhu ni kuwaumiza wakulima, wanaotarajia majibu ya Serikali ili walime, wavune chakula na kuuza mazao yao kwa Usalama wasomeshe.
 
“Wakulima wanapopewa majibu mepesi kwa maswali magumu, wanahisi hawana Viongozi wa Serikali wanaomsaidia Rais, na kudhani hana watu wa kumsaidia kujibu hoja za msingi, hasa wakati huu wa Mkakati wa Matokeo ya Haraka sasa (big results now strategy)
 
Mbali ya Swali la Mgogoro wa Wakulima na Wafugaji, Mengine ni kuhusu za Fedha za Mfuko wa Jimbo, Makalla alisema yeye ni Mjumbe hana Majibu, Ahadi ya Ujenzi wa Zahanati alisema anangoja aone Juhudi za Wananchi atawasaidia, na kusuasua kwa Mradi wa Maji (PADEP) ambao alisema atafuatilia maana si Mhandisi.
 
Aidha Katibu wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Sungaji Shukuru Mikenegeze alisema, “Kama ulivyomsikia Mbunge, Wafugaji wana Nguvu ya Fedha, hivyo itabidi na sisi tuanzishe vikundi vya Kijamii kulinda mazao yetu yasiharibiwe na mifugo, jambo ambalo watu wanadai itaibuka Vita.

No comments:

Post a Comment

Pages