HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 12, 2013

WALTER AMPIGA TAFU GODZILLA

Na Elizabeth JohnRAPA wa Muziki wa Hip Hop nchini, Tzee Godzilla ‘Godzilla’, amesema anatarajia kuachia ngoma yake mpya hivi karibuni inayokwenda kwa jina la ‘Thanks God’.


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, rapa huyo alisema ngoma hiyo ameshirikiana vyema na msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Walter Chilambo.

Alisema maandalizi ya ngoma hiyo yapo katika hatua za mwisho na muda wowote anaweza kusambaza katika vituo mbalimbali vya redio kwa ajili ya kuburudisha na kuelimisha jamii.

Alisema katika kuhakikisha kibao hicho kinakuwa na ladha mchanganyiko ameamua kumshirikisha Walter huku akiwataka mashabiki kumpa ushirikiano zaidi ili aweze kufanikisha malengo yake ya kuwapa burudani.

“Ninaimani uwepo wa msanii huyo katika kazi yangu utasaidia mambo mengi katika kuhakikisha ngoma hiyo inafanya vyema katika anga za muziki ninaofanya,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages