HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 29, 2013

DC Mtaka atoa siku 7 wafugaji kuhama kwa hiari, 14 kwa lazima

Na Bryceson Mathias, Mvomero
MKUU wa Wilaya ya Mvomero, Antony Mtaka, jana ametoa siku 7 kwa wafugaji waliovamia Tarafa ya Turiani kuhama kwa hiari yao na siku 14 kuhama kwa lazima, kutokana mapigaano yanayoendelea baina ya Wakulima na Wafugaji na Jamii ya Kimasai na Wamang’ati.
Kauli ya Mtaka imekuja siku chache kufuatia ahadi aliyoitoa baada ya Maandamano ya Wakulima yaliyofanywa hivi karimu ambapo wakulima wa Kitongoji cha Dibigwa na Kijiji cha Kisala Kata ya Sungaji, waliandamana kwenda Kituo cha Polisi Turiani na Kufunga Barabara.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Hoteli ya Queen Park Manyinga toka saa 6 hadi saa 8 mchana, ukiyahusisha makundi ya wakulima, wafungaji, viongozi na Madiwani wote watano wa Tarafa ya Turiani, Mtaka alitoa tamko la serikali la kuwataka wafugaji kuhama eneo la wakulima kwa hiari yao ndani ya siku 7, na siku 14 kwa lazima.
“Ili kunusuru maafa baina ya wakulima na wafugaji, uharibifu wa mazao, na mapigano ya Wafugaji wa Kimasai na jamii ya Kimang’ati dhidi ya Wakulima, Serikali inatoa amri ya wafugaji waliovamia maeneo Kilimo kuhama kwa hiari ndani ya siku 7 na 14 kwa lazima” alisema Mtaka.
Aidha Mtaka aliwaonya Wakulima wanaaowakaribisha wafugaji na kuwauzia maeneo, majani au Mabua, na kwamba wakifahamika watachukuliwa hatua kali kwa sababu wao ndio vya kusababisha migogoro miongoni mwa jamii hiyo kutokana na uroho wa kipato.
Hata hivyo baada ya Kikao hicho Mtaka aliongozana na Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kwenda kwenye eneo la Mapigano yaliyozuka baina ya Wafugaji wa Jamii ya Kimang’ati na ile ya Kimasai ambayo yametokea katika Vitongoji vya Kivungwe, na Masangarawe

No comments:

Post a Comment

Pages