HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 29, 2013

YOSO LINDI SOCCER ACADEMY AFARIKI DUNIA

Marehemu Exavel Richard (wa kwanza kushoto waliokaa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na kikosi cha Lindi Soccer Academy (LSA) nje ya Hotel Double M, ilikokuwa imeweka kambi kujiandaa na michuano ya Copa Coca Cola mwezi uliopita. Kushoto (waliosimama) ni Ofisa Habari wa LSA, Salum Mkandemba alipotembelea kambi hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Hafidh Karongo na Meneja wa Double M aliyekaa mbele yake.

LINDI, Tanzania

Kabla na baada ya mazishi ya Exavel, wadau, viongozi, wachezaji na wazazi wa wachezaji wa LSA wanakutana katika Hoteli ya Double M mjini Lindi, kuratibu shughuli za mazishi hayo yaliyofanyika kwenye Makaburi Msafa saa 10 alasiri jana

TIMU ya Lindi Soccer Academy (LSA) ya mjini Lindi, imepata pigo kutokana na msiba wa ghafla wa mchezaji wake Exavel Richard, aliyefariki jana jioni katika Hospitali ya Sokoine, alikokuwa amekimbizwa kwa matibabu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa LSA, Hafidh Karongo, Exavel aliyekuwa tishio katika nafasi ya ulinzi wa kushoto, kiungo-mkabaji na winga wa kushoto, alikutwa na mauti katika hospitali hiyo ya mkoa, alikokimbizwa baada ya kulalamika maumivu ya kichwa.

Karongo alibainisha kuwa, baada ya Jumanne jioni kurejea kutoka shule, Exavel alidai kuumwa kichwa, maumivu yaliyoendelea hadi Jumatano, ambapo alikimbizwa hospitalini hapo na kufariki saa chache baadaye.

“Alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Wailes, ambapo Jumanne alikuwa na testi kujiandaa na mitihani ya taifa, alirejea nyumbani huku akidai kuumwa kichwa, ambapo asubuhi ya Jumatano alikimbizwa hospitali alikofariki,” alifafanua Karogo.

Exavel ambaye mechi yake ya mwisho kuichezea LSA ni ile ya kirafiki dhidi ya Mkwaya Boys iliyopigwa Agosti 11, ambayo alicheza kwa dakika 30, atakumbukwa kwa mchango wake katika mechi 32 alizoichezea, akibeba mataji matatu likiwamo la Lindi Street Soccer.


Kabla na baada ya mazishi ya Exavel, wadau, viongozi, wachezaji na wazazi wa wachezaji wa LSA walikutana katika Hoteli ya Double M mjini Lindi, kuratibu shughuli za mazishi hayo yaliyofanyika kwenye Makaburi Msafa saa 10 alasiri jana.

No comments:

Post a Comment

Pages