HABARI MSETO (HEADER)


September 30, 2013

ITIKADI ZA CCM NA CHADEMA ZAKWAMISHA UJENZI WA STENDI
Na Bryceson Mathias, Manyinga
KAMATI ya Ulinzi na Usalama Mvomero, ina Kibarua kigumu kutatua Mgogoro wa Viongozi na Wakazi wa Manyinga Diongoya, wanaopimana Msuli na Viongozi wa Andiko la Mradi wa Stendi Community Facilitation Centre (CFC), unaokwamishwa na Itikadi za Vyama vya siasa vya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Viongozi wa Mradi huo wa CFC wametajwa kuwa ni Mwenyekiti wa andiko hilo, Feruz Pessa, Katibu, Mwalimu Rashid Juma Idd, Mkazi wa Mtibwa, na Mjumbe, Dismas Ngeresha, Mkazi wa Manyinga, ambapo upekuzi umedai ni Wapenzi na Wanachama wa CHADEMA.
Wakifanya upelelezi huo jana kuhusiana na Mradi huo, Askari Edward Maende akiongozana na Askari Mwenzake ambaye hakujitaja jina , walimhoji Mtu mmoja iwapo ni mmoja wa walioomba kupewa vibanda vya Ujenzi katika Stendi hiyo, kitu kinachoakisi Mgogoro huo.
“Tumetumwa na OCD-CID wa Wilaya Majengo, utupe maelezo unafahamu nini kuhusu kuomba kwako Kibanda eneo linalozunguka Stendi ya Mabasi Manyinga, na kama ulilipia ni kiasi gani cha fedha ulitoa na lini?”.alisema Askari mpelelezi Mahende.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi, OCD-CID Majengo alithibitisha kuwatuma Askari hao, akikiri wana taarifa za kutoelewana kati ya Viongozi wa Kijiji hicho kwa niaba ya wananchi na CFC, ambapo ilidaiwa wamekiuka makubaliano ya Mkataba na muda wao umepita.
Uchunguzi uliofanywa unaonesha kuna Mdudu wa Kisiasa amejipenyeza na kungilia mchakato  huo ambapo imebainika Kigogo mmoja anarumbatana na waandishi wa andiko hilo toka  CHADEMA, wanaopingana wa wale wa CCM ni nani hasa anahusika na Mradi huo.
Aidha imedaiwa kuna wananchi walitapeliwa Maelfu ya Fedha, ikielezwa CFC walitakiwa kubaki kama waandishi wa andiko la Mradi wa Stendi na si wagawaji wa Viwanja, nacho Kijiji kikiona ndicho kilitakiwa kugawa viwanja, huku kila upande ukijipatia fedha bila maridhiano.

No comments:

Post a Comment

Pages