HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 24, 2013

MAGAIDI SITA WA AL SHABAAB WAUAWA WESTGATE

NAIROBI, Kenya
Vikosi vya usalama nchini Kenya vinasema viko katika mkondo wa lala salama katika kuweza kudhibiti jengo zima la Westgate. 
Hadi sasa serikali inasema kuwa mateka wote wameokolewa huku wanamgambo sita waliosalia wakiuawa usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa usalama idadi kamili ya magaidi waliouawa ni tisa .

Duru kutoka shirika la AFP zinasema kuwa majeshi ya Kenya yangali yanakabiliana na gaidi mmoja au wawili ambao wamesalia ndani ya jengo la Westgate.

Inaarifiwa magaidi hao walijitawanya wakiwa ndani ya jengo hilo kila mmoja akijificha sehemu yake katika ghorofa ya juu zaidi ya jengo hilo.

Milio ya risasi na milipuko ilisikika mapema leo asubuhi kutoka katika jengo hilo.

Ukabilianaji huo ulitokea baada ya serikali ya Kenya kutangaza kudhibiti jengo hilo zima huku hali hiyo ikishuhudiwa kwa siku ya nne.
Serikali ilisema kuwa mateka wote wameokolewa ingawa bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu hali ilivyo sasa.

No comments:

Post a Comment

Pages