Na Elizabeth John
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limependekeza majina ya wanariadha zaidi ya 30 watakaounda timu ya taifa inayotarajia kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola mwakani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu
Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui, alisema vijana hao wanatarajiwa kuingia kambini
Desemba Mosi, mwaka huu kwaajili ya mashindano hayo.
Alisema lengo la kuwapeleka kambini wanariadha hao ni kuwanoa kwaajili ya mashindano hayo na kwamba hawataki kurudia yaliyotokea katika mashindano ya Dunia.
Alisema wameandaa mipango ambayo wanatarajia kuipeleka Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kwaajili ya kuhakikisha vijana waliochaguliwa kuweza kutoka nje ya nchi kwaajili ya kufanya majaribio kwaajili ya kuwapata wanariadha wazuri zaidi watakaoweza kufika Uingereza.
“Mashindano
ya Jumuiya ya Madola yatafanyika Agosti, mwakani nchini Uingereza, hivyo
tumejipanga kikamilifu kuhakikisha tunawanoa wanariadha wetu,” alisema Nyambui.
“Sio
wote 30 waliochaguliwa wanaweza kwenda kushiriki mashindano hayo kutakuwa na
mchujo ambao utafanyika katika mashindano mbalimbali hapo baadae,” alisema.
No comments:
Post a Comment