Na Elizabeth John
NYOTA wa muziki
wa kizazi kipya nchini, Ismail Seif ‘Suma Lee’ anajipanga kuachia kazi yake
mpya hivi karibuni ambayo bado hajaipatia jina kutokana na ubora wa kazi hiyo.
Suma Lee
alishawahi kutamba na kazi zake kama, ‘Utanikumbuka’, ‘Hakunaga’, ‘Chungwa’ na
nyinginezo ambzao zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa
kizazi kipya nchini.
Kwa mujibu wa
Suma Lee, kazi hiyo ameshaindaa kilichobaki ni kuipa jina na kuisambaza katika
vituo mbalimbali vya redio.
“Nashindwa niipe
jina gani hazi hii kutokana na ubora ulionao nimejaribu kuwashirikisha wasanii
wenzangu wanisaidie lakini kila mmoja anaupa jina lake, tutakubalina na
kuchagua lililo bora zaidi,” alisema.
Alisema anaomba
mashabiki wake wakae mkao wa kula kwaajili ya kazi hiyo ambayo anaamini
ataisambaza ikiwa pamoja na video yake ili kuwapa burudani iliyokamilika
mashabiki na wapenzi wa kazi zake.
No comments:
Post a Comment