Washtakiwa watatu kati ya watano waliokuwa
wakikabiliwa na kesi ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya
Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wamehukumiwa kifungo
jela baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwatia hatiani ambapo kati yao
ni mke na mume. Kushoto ni Bahati John amehukumiwa kifungo cha miaka 7 na
katikati ni Manase Mwakale amehukumiwa miaka 5 na mkewe Eddah Mwakale
amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja.
Manase Mwakale akiongea na wakili wake baada ya
kuhukumiwa kifiungo cha miaka mitano jela.
Eddah Mwakale akiongea na wakili wake. Kulia ni Mume wake, Manase Mwakale ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela.


No comments:
Post a Comment