Askofu Mkuu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dk. Alex
Malasusa akimpa mkono mmoja wa watoto waliohudhuria ibada ya Krismasi katika Kanisa
la Azania Front jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Francis Dande)
Baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki wakiwa katika ibada ya Sikukuu ya Krismasi
katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.
Watoto
wakisoma biblia wakati wa ibada ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa la
Azania Front.
Kwaya
Kuu ikiimba nyimbo za kumsifu Mungu, wakati wa ibada ya Krismasi iliyofanyika
katika kanisa la Azania Front Dar es Salaam.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dk. Alex Malasusa akimbariki mtotoTikisaeli Shoo mara baada ya
ibada ya Krismasi kumalizika kanisani hapo.
Na Mwandishi Wetu
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la
Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front, Alex Malasusa,
amewataka viongozi kuacha tabia ya ubinafsi na rushwa kwa kujilimbikizia mali
huku waliowengi wakiishi katika lindi umasikini.
Kauli hiyo aliitoa, wakati
alipokuwa akizungumza na waamini kwenye ibada
ya kusherehekea kuzaliwa Yesu Kristo, iliyofanyika leo kwenye Kanisa hilo
jijini Dar es Salaam.
Alisema kutokana, ubinafsi,
rushwa na tawala za kijanja, janja kama
zile za enzi ya Herodi, zimefanya dunia kutawaliwa, maovu kila kona pamoja
kulipizana visasi.
“Dunia hii leo imejaa maovu
kila kona, watu wanatumia hela nyingi kwa ajili ya kujipatia silaha za kivita
hali hiyo inatokana na watu kutotaka kuishi kwa amani”alisema Askofu Malasusa.
Askofu Malasusa, alisema kuna
watu wako tayari kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kununua silaha za kulinda
madaraka na kulipiza kisasi.
“Huu ni wakati wa jamii
kuwaepuka baadhi ya watu ambao hawapendi kuwaona watu wakiishi kwa mshikamano
na amani”alisema Askofu Malasusa.
Aliongeza kuwa wataka
viongozi hao wakisherehekea siku kuu hiyo, ni lazima watumie nyadhifa zao za
kiserikali kutenda haki na kusimamia maendeleo ya kiuchumi katika jamii.
Aidha, amewakemea baadhi ya
viongozi wa dini ambao wamekuwa wakitoa mafundisho mabaya kwa watu ili waitumie
vibaya dini, hivyo ni lazima waamini waishike imani yao na wasikubali
kupotoshwa.
Naye Askofu Msaidizi Mkuu wa
Jimbo Kuu la Wakatoliki, Dar es Salaam, Dk Eusebius Nzigilwa, alishangazwa na
tabia ya baadhi ya watu pindi wapatapo uongozi kushindwa kupigania haki na
baadala yake wanajikusanyia mali huku wakiwaacha waliowengi wakitaabika kwa
masikini.
“Hata hapa wapo viongozi hao
wanaopenda kujilimbikizia mali kwa ajili ya maslahi binafsi pamoja na rafiki
zao”alisema Dk Nzigilwa.
Dk Nzigilwa alisema wanataka
kuwaona watu ambao wako tayari kupoteza nyadhifa zao kwa ajili ya kupigania
haki ya waliowengi
“Na ndio vyo viongozi wetu
wanatakiwa kufanya, kwa kuzitumia nafasi zenu kutasaidia kuinua maisha katika
jamii mfano alivofanya Yesu ”.
Aidha, aliwataka watanzania
kudumisha amani na mshikamano hasa wakati wa hatua hii ya nchi kuelekea kwenye
mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Dk Nzigilwa alisema
anatarajia mambo yatakayoingizwa kwenye katiba hiyo yatakuwa ni yale
yatakayoleta haki katika kusimamia rasilimali kwa ajili ya kukuza ustawi wa
kila mmoja katika Tifa hili.
No comments:
Post a Comment