HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 26, 2013

MWANAFUNZI WA CBE-DODOMA AFARIKI DUNIA
MAREHEMU  SAMWEL P. KITULA

Ikiwa ni siku moja  imepita Tangu Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dodoma  kiondokewe na aliye wahi kuwa Mwanafunzi wa Chuo hicho katika Level ya Diploma 2012/2013 Marehemu Zeinabu J. Kasenga (ODMK -2012/2013)

Simanzi zimezidi kutanda Chuoni  hapa baada  ya Mwanafunzi Mwingine  Bw. Samwel P. Kitula (37)  aliyekuwa  akisoma  Bachelor Degree  in  Procurement and Supplies Management  mwaka wa tatu (3) mkondo  "A"  Kufariki Dunia usiku wa  kuamkia Tarehe 26/12/2013  ( Mnamo saa 8 usiku)  katika hospitali ya  Mkoa wa Dodoma (General Hospital).

Kwa mujibu wa Msemaji wa Familia   amesema  Marehemu   alikuwa akisumbuliwa na Matatizo  ya Ini mpaka kupelekea Mauti yake.

Kwa upande wake Rais wa Serikali ya wanafunzi  wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Dodoma Mhe. Remidius  M. Emmanuel  amesema  Amepokea taarifa hiyo kwa majonzi makubwa sana  na kuwataka wanafunzi wote kuwa wavumilivu  hasa katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza  mwanafunzi mwenzetu. Hata hivyo Rais huyo amewataka  wanafunzi  kuwa  watulivu  wakati taratibu mbalimbali  zinaendelea  na kila kitakachoendelea watafahamishwa  kupitia taratibu  mbalimbali za  mawasiliano hapa chuoni.Ingawa  amasema Marehemu amekuwa akiishi na familia yake eneo la Makole  karibu kabisa na Lodge ya ELGON, hivyo ni vema  kila mtu kwa nafasi yake kujongea  eneo hilo kwa ajili ya kutoa pole kwa Familia ya Marehemu.

No comments:

Post a Comment

Pages