Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka tanzania (TFF), Boniface Wambura akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu elimu watakayotoa kwa mashabiki wa soka juu ya mfumo mpya wa matumizi ya tiketi za kielekroniki. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi TFF, Salum Madadi.
DAR ES SALAAM,Tanzania
DAR ES SALAAM,
SHIRIKISHO la Soka Tanzania
(TFF), kwa kushirikiana na Benki ya CRDB, wamejipanga kutoa elimu kwa mashabiki
wa soka nchini juu ya mfumo mpya matumizi ya tiketi za Kielektroniki
zinazotarajiwa kuanza kutumika rasmi katika raundi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania
Bara.
CRDB ndio wazabuni
walioshinda tenda ya kuuza aina hiyo ya tiketi, ambazo mpaka sasa zimeanza
kufanyawiwa majaribio ya mauzo katika mechi ya Azam FC, dhidi ya RuvuShooting kwenye
Uwanja wa Chamazi wiki iliyopita.
CRDB kwa kushirikiana na TFF,
leo inatarajia kuendelea na mxchakatop wa majaribio ya mauzo ya tiketi, kupitia
pambano la kirafiki maalum kwa ajili baina ya Ashanti United dhidi ya Maafande wa
JKT Ruvu.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface
Wambura alisema hayo leo kuwa, wameamua kufanya hivyo kutokana na uelewa mdogo
wa baadhi ya mashabiki wa soka, uliodhihirika na mechi ya awali ya majaribio ya
tiketi hizo.
Wambura alisema, elimu hiyo
itatolewa kwa kina, kwani wamegundua watu hawajui nini maana ya tiketi hizo
kwani katika mchezo uliopita walipata wakati mgumu juu ya suala hilo .
“Mchezo uliopita dhidi ya
Azam FC na Ruvu Shooting, TFF na CRDB tulipata wakati mgumu mara baada ya
mashabiki kuja na pesa zao uwanjani wakijua tiketi hizo zinapatikana pale moja
kwa moja - wakati sio hivyo,” alisema Wambura.
Aliongeza kuwa, TFF
inaangalia uwezekano wa kuwapa semina waandishi wa habri ili waweze kufikisha
ujumbe kwa umma juu ya matumizi sahihi ya mfumo huo wa tiketi za kielektroni.
No comments:
Post a Comment