Makamu wa
Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akimkabidhi cheti Naibu Mkurugenzi
Mtendaji-Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka kutokana na mchango
wa benki hiyo katika kufanikisha sherehe za utoaji wa Tuzo za Mwajiri Bora wa
Mwaka (EYA 2013), ambapo benki hiyo ilikuwa moja ya wadhamini katika hafla hiyo
iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia
Kabaka (kushoto) akimkabidhi,
Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka
Tuzo ya Fedha ya ushindi wa pili ya Mwajiri Bora wa Mwaka (EYA 2013),
zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa
Rasilimali Watu wa benki hiyo, Timoth Fasha. Sherehe hizo zilifanyika jijini
Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Benki ya CRDB, ilikuwa pia Mdhamini wa Fedha (Gold Sponsor) wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa waajiri bora, ambapo ilikabidhiwa cheti
cha udhamini.
Kaimu Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela akipeana mkono na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka akipeana mkono na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kushoto), akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi wa Rasirimali Watu wa Benki ya CRDB, Timoth Fasha.
Mkurugenzi wa tawi la Lumumba, John Almasi (kulia), Mkurugenzi wa tawi la Kijitonyama, Lucas Busigaz, Mkurugenzi wa tawi la Vijana, Peres Fungo, na Mwanasheria wa Benki ya CRDB wa pili kushoto na Ofisa Uhusiano wa Benki ya CRDB, Tumain Kamuhanda.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka akizungumza na waandishi wa habari. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa benki hiyo, Timoth Fasha.DAR ES SALAAM, Tanzania
BENKI ya CRDB imefanikiwa kutwaa Tuzo ya Mwajiri
Bora wa Mwaka 2013 (EYA), iliyotolewa na
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika jijini Dar es Salaam, hivyo
kuendelea kuwa kinara miongoni mwa waajiri wa taasisi za fedha.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Naibu Mkurugenzi
Mtendaji-Huduma Shirikishi, Esther Kitoka, alisema CRDB inajivunia kiwango
chake katika kuwajali na kuwathamini wafanyakazi, hivyo kuwawezesha kutwaa tuzo
hiyo mara pili mfululizo.
Aliongeza kuwa, ili kuhakikisha wanafanikiwa kutwaa Tuzo ya Mwajiri Bora (EYA), ambayo mwaka huu imechukuliwa na Kampuni ya Simu ya Vodacom,
wamejipanga kuboresha maafunzo miongoni mwa waajiriwa wao ili kuwaongezea ufanisi
kazini.
“Mwakani tutakuwa na mafunzo ya wafanyakazi wetu katika Chuo
Kikuu cha Milpark cha Afrika Kusini, ili kuboresha ufanisi miongoni mwa
wafanyakazi na kurutubisha CV zao, vyote vikiwa ni kwa ustawi wa Benki CRDB na wateja
wetu kwa ujumla,” alisema Kitoka.
Kitoka akasisitiza kuwa, kupitia mikakati hiyo, wanaamini
mwakani Benki ya CRDB wataibuka washindi wa jumla (overall), hasa baada ya kutanua
huduma zake hadi nje ya nchi kupitia matawi yake nchini Burundi na huduma za
China UnionPay na China Desk.
Kwa upande wake Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka
aliwapongeza washindi wote waliotwaa tuzo katika hafla hiyo, huku akiwataka
kuboresha mazingira ya kazi miongoni mwa waajiriwa, kama ishara ya kuthamini
mchango wao kwa kampuni na taifa.
Kabaka aliongeza kuwa, mhimili mkuu wa ukuaji wa uchumi wa
nchi yoyote duniani ni utendaji uliotukuka miongoni mwa waajiriwa wa sekta
rasmi na isiyo rasmi, ambao wasipoboreshewa mazingira, hawatokuwa wazalishaji
wazuri kwa ustawi wa taifa.
Awali akifungua hafla hiyo, mgeni rasmi, Makamu wa Rais Dk
Mohammed Gharib Bilal, aliwataka waajiri wote nchini kutumia hafla ya tuzo za
Mwajiri Bora kama nia ya kujibu maswali lukuki kuhusu uzalishaji wa bidhaa na
utawala bora mahali pa kazi.
Jumla ya tuzo 21 zilitolewa kwa kampuni mbalimbali
zilizoshiriki katika mchakato huo uliokuwa chini ya udhamini mkuu wa Ultimate
Security (Platinum Sponsor) na benki ya CRDB (Gold Sponsor) na kuratibiwa na
ATE.
No comments:
Post a Comment