MASHABIKI VASCO DA GAMA, ATLETICO PARANAENSE WATWANGA
Shabiki aliyejeruhiwa vibaya akiwa amelala kwenye machela kusubiri msaada.
Shabiki wa Atletico Paranaense akikanyagwa na kupigwa mateke na mashabiki wa Vasco da Gama.
Shabiki mwingine akitolewa na machela kwenda kupakizwa kwenye helikopta awahishwe hospital.
Polisi wakipiga mabomu ya machozi kumuokoa shabiki kwa kuwatawanya waliokuwa wakimshambulia.
Mmoja wa mashabiki waliojeruhiwa, akishushwa kutoka jukwaani akiwa kwenye machela.
Mmoja wa majeruhi akikimbizwa na gari maalum kwenda ilikopaki helikopta.
Helkopta iliyotua uwanjani kuchukua majeruhi kupeleka hospitali.
Beki wa Atletico Paranaense, Luiz Alberto akilia baada ya kuona shabiki wa timu yake alivyopigika na kuumizwa vibaya.
RIO DE JANEIRO , Brazil
"Nimecheza soka
kwa miaka 20 na sijawahi kuona ukatili kama
huu kwa mtu mmoja. Tutakuwa wenyeji wa Kombe la Dunia mwakani na tunapaswa
kujua kuwa taswira ya vurugu hizi itaonekana duniani kote"
MSIMU wa soka wa ligi ya hapa ulifikia tamati Jumapili kwa
vurugu kubwa uwanjani, ambako watu watatu walijeruhiwa vibaya, huku klabu mbili
kubwa zikiporomoka daraja la Ligi Kuu hadi Daraja la Kwanza .
Mecho moja ya Ligi Kuu ilisimamishwa kwa lisaa limoja Kusini
mwa hapa Brazil ,
baada ya kuzuka mapigano makali baina ya mashabiki wa klabu mbili za Vasco da
Gama na Atletico Paranaense.
Picha za televisheni zilimuonesha mtu mmoja akipokea
mkong’oto wa mateke ya kichwa kutoka kwa mashibiki, ambaye alikuja kuokolewa,
kisha helikopta iliitwa na kutua sehemu ya kuchezea na kumpakiza majeruhi huyo
kwenda hospitali.
Vyombo vya habari vya hapa vimeonesha shaka kuwa ukatili wa
kutisha ulioambatana na vurugu hizo, zilizokuwa zikirushwa moja kwa moja, zimeitia
doa Brazil
kuelekea fainali zijazo za Kombe la Dunia zitakazopigwa hapa.
Vurugu hizo zilifanywa na mashabiki kwenye Uwanja wa Arena
Joinville, ulioko katika Jimbo la Kusini la Santa Catarina, kuanzia dakika ya
16 ya pambano hilo ,
ambako mchezaji mmoja wa Atletico Paranaense aliangua kilio baada kushuhudia
kipigo hicho cha shabiki.
"Nimecheza soka kwa miaka 20 na sijawahi kuona ukatili kama huu kwa mtu mmoja. Tutakuwa wenyeji wa Kombe la
Dunia mwakani na tunapaswa kujua kuwa taswira ya vurugu hizi itaonekana duniani
kote," alisema beki Luiz Alberto kuwaambia wanahabari.
Katika mechi hiyo, Vasco da Gama walihitaji ushindi katika
mechi hiyo ili kubaki katika soka la daraja la juu hapa Brazil , Lakini licha ya umuhimu wa
mechi hiyo hakukuwa na askari uwanjani hapo, zaidi ya vikosi vya ulinzi
vilivyokodiwa.
BBC Sport/Goal.com
No comments:
Post a Comment