Msama akisaidia kushusha vitu katika gari.
Picha ya pamoja.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Krismasi, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula mlezi wa kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni jijini Dar es Salaam, Halima Mpeta.
Mlezi wa Kituo cha Yatima cha Malaika Kids, Mwanaid Ramadhani akipokea zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya kutoka kwa Msama.
Picha ya pamoja.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Krismasi, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula mlezi wa kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni jijini Dar es Salaam, Halima Mpeta.
Mlezi wa Kituo cha Yatima cha Malaika Kids, Mwanaid Ramadhani akipokea zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya kutoka kwa Msama.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha
la Krismasi, Alex Msama akimkabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka
Mpya, mlezi wa kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Yatima
Group cha Mbagala Chamanzi jijini Dar es Salaam, Haruna Mtandika. Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Jumla ya vituo vitano vilinufaika na
msaada wa sukari, unga, mafuta, sabuni pamoja
na mchele. (Picha na Francis Dande)
Na Francis Dande
KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la
muziki wa injili la Krismasi litakalozinduliwa kesho Uwanja wa Taifa chini ya
uratibu wa kampuni ya Msama Promotions, jana walitoa msaada wa vitu mbalimbali kwa vituo vitano
vya yatima vya jijini Dar es Salaam .
Akikabidhi msaada wa vitu hivyo vyenye
thamani ya shilingi mil 5, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya maandalizi, Alex Msama
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, alisema fedha hizo zimetoka
kwenye mfuko wa Tamasha hilo
linalofanyika mara ya kwanza.
“Tumeamua kutoa msaada huu kwa yatima
kutokana na kuguswa na hali yao hasa katika kipindi hiki cha kuelekea sikuu ya
Krismasi, tumeamua kutoa hiki kidogo ili nao wajisikie furaha kama watoto
wengine wenye wazazi wao,” alisema Msama.
Msama alisema japo ni mara ya kwanza
kufanyika kwa Tamasha hilo la Krismasi tofauti na lile la Pasaka ambalo
liliasisiwa mwaka 2000, bado wakaona watoe kiasi kidogo wakiamini watoto
watafarijika katika sikukuu hiyo.
Vituo vilivyopata misaada hiyo ya
kiutu ambayo ni pamoja na Mwandaliwa cha Mbweni, Mahabusi ya Watoto jijini Dar
es Salaam, Yatima Group cha Mbagala, Malaika Kidds cha Mwananyamala na kingine
ambavyo jumla yake ni vitano.
Akipokea msaada huo jana katika Ofisi
za Dira Mtanzania Publishers Ltd, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Ofisa
Mfawidhi wa Mahabusi ya Watoto, Ramadhani Yahya, alishukuru na kuwataka wengine
waige mfano wa Msama kuyakumbuka makundi maalumu katika jamii.
Naye Halima Mpeta wa Kituo cha
Mwandaliwa cha Mbweni, alisema anashukuru kwani msaada huo sio tu umekuwa
faraja kwa kituo hicho na watoto, pia umekuja wakati muafaka kuelekea Krismasi
ambapo ni faraja kubwa kwa watoto hao wenye mahitaji.
Msama amekabidhi misaada hiyo ikiwa ni
siku mbili kabla ya uzinduzi wa Tamasha la Krismasi litakalofanyika kesho
kwenye Uwanja wa Taifa ambapo waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania, watahudumu.
Waimbaji wa Tanzania, ni Rose Muhando,
Upendo Mkone, Upendo Kilahilo, Edson Mwasabwite, John Lissu na New Life
Band.
Kutoka nje ni Solly Mahlangu kutoka
Afrika Kusini, Solomon Mukubwa (Kenya ),
Liliane Kabaganza na Ephraim Sekeleti kutoka Zambia ambao walishaanza kutua
nchini tangu juzi.
Msama alisema, mbali ya malengo ya
msingi ya tamasha hilo ambayo ni kueneza injili kwa mataifa yote kupitia vipaji
vya uimbaji, sehemu ya mapato yataelekezwa katika ujenzi wa kituo cha yatima
kitakachojengwa eneo la Pugu, jijini Dar
es Salaam .
No comments:
Post a Comment