HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 13, 2013

SBS yazindua kadi ya B-PESA katika soko la Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa Smart Banking Solutions Limited (SBS) Gustavo Vermaas (kulia), Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania, Jaji mstaafu Thomas Mihayo (wa pili kulia), Mkuu wa Maendeleo ya Biashara, Elibariki Lukumay (wa tatu kulia) na Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Edmund Mdolwa wakikata keki wakati wa uzinduzi wa kadi ya malipo ya kabla ya kielektroniki ya daraja la juu inayotumia mfumo wa kibenki ijulikanayo kama B-PESA. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Smart Banking Solution Ltd (SBS) imezindua kadi ya malipo ya kabla ya kielektroniki la daraja la juu inayotumia mfumo wa kibenki ijulikanayo kama B-PESA, ambayo ni ya kwanza na ya aina yake katika soko la kibenki la Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kuzindua kadi hiyo ya B-PESA katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Jumatano jioni, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya SBS, Gustavo Vermaas alisema kuwa kadi hiyo inamuwezesha mteja kufanya muhala katika benki yoyote mwanachama wa B-PESA au wakala wowote wa B-PESA au katika ATM za B-PESA ambazo zimeanza kusambazwa nchini kote.

“Kadi hii inakuwezesha kuwa na urahisi wa kufanya mihala ya kadi kwenda kadi nyingine, kutoa fedha, kuweka, na kulipia bili mbali mbali. Kadi ya B-PESA si kadi inayotoa huduma zinazoendana na mikopo, na haijaunganishwa na akaunti ya benki ya mteja.

“B-PESA ni kadi iliyosalama na yenye chipu pamoja na mstari mnaso inayokulinda dhidi ya wezi wakutimia teknologia, ni salama kwa kuwa haunahaja ya kubeba fedha taslim, ni rahisi kwa kuwa kuna mtandao wa benki wanachama wa B-PESA na mawakala wa B-PESA ambapo unaweza ukafanya muamala wakati wowote, ikiwa haina usumbufu wowote kwani unatumia kile ulichonacho kwenye kadi na haikuingizi katika madeni na ni rahisi kupata kadi ya B-PESA,” alisema Bw Vermaas.

Vermaas alisema kuwa uanzishwaji wa kadi ya B-PESA utasaidia kupunguza mzunguko wa fedha taslimu katika solo la Tanzania na kuibadilisha jamii ya watanzania kuwa jamii isiyotumia fedha taslimu, pale matumizi yake itakapoenea nchini kote.

Alibainisha kuwa kampuni yake imeingiza sokoni kadi ya B-PESA kwa ajili ya malipo yote kwa ujumla, kadi ijulikanayo kama Kadi ya Mafuta (Mafuta Card) kwa madereva au watumiaji wa mafuta na Kadi ya Ada yaani (Ada Card) kwa ajili ya malipo ya ada ya shule.
“Pia tuna kadi ya B-PESA ya Mshahara na Kadi ya Mafao zikiwa njiani ambazo wastaafu watakuwa wakipokea malipo popote walipo,” aliongeza.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya SBS, Bw Edmund Mdolwa akizungumza katika tukio hilo alisema bidhaa ya B-PESA ni kadi na pia ni pochi linalotembea ambayo ukidhi matakwa ya wateja wenye mapato madogo na hata wale wafanya biashara wakubwa.

“Unaweza fanya muamala au kufunga kadi hii endapo unahisi kimeibiwa, kwa kupitia simu yako ya mkononi au kwa kutumia mtandao (Computer). B-PESA ni kadi inayoleta suluhisho ya malipo katika jamii yetu kwa ujumla bila kuwa na matabaka,” alisema Mdolwa.
Mdolwa alisema uanzishwaji wa mfumo huu wa malipo utakuwa na faida kubwa kwa Tanzania kwa kuwa wafanyabiashara wake hawatohitaji kutafuta fedha za kigeni wakinunua bidhaa nchi za nje, kwa sababu kadi ya B-PESA sasa itakuwa inakubalika katika vituo vyote vya UnionPay dunia nzima, baada ya kusaini makubaliano ya ubia na UnionPay wakati wa uzinduzi.
Taasisi nyingi za kibenki zimeeleza nia ya kushirikiana na SBS ili kuaza utoaji wa kadi za B-PESA kwa wateja wake, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Commercial Bank of Africa (Tanzania) , Yohane Kaduma, alisema benki yake itaanza kutoa huduma hiyo kwa wateja wake hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Pages