HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 13, 2013

WATU SABA WAFUKIWA NA KIFUSI NA KUFA PAPO HAPO-MOSHI
Wananchi wakijaribu kufukua udongo ili kuopoa  miili ya watu walofukiwa na kifusi katika machimbo ya Moramu eneo la Pumuani wilaya ya Moshi vijijini huku wananchi wengine wakishuhudia. Tukio hilo limetokea usiku jana na zoezi kudumu la kuopoa miili lilidumu hadi saa nane usiku. (Picha zote na Dixon Busagaga)



 Uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro ukiongozwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama ukishuhudia zoezi la ukoaji wa miili ya watu hao.
 Mmoja ya mwili wa mmoja kati ya watu sita waliokufa kwa kufunikwa na kifusi katika machimbo ya Moramu eneo la Pumuani wilaya ya Moshi vijijini.
 Gari aina ya fuso lenye namba za usajili T 167 AQG ambalo marehemu wa tukio hilo walikuwa wakijaza Moramu likiwa limeangukiwa na ngema iliyokatika na kusababisha vifo vya watu sita.
 Miili ya baadhi ya watu waliofunikwa na kifusi ikiwa inafanyiwa

utaratibu wa kwenda kuhifadhiwa.

 Miili ya baadhi ya watu waliofunikwa na kifusi.

 Miili ikiopolewa.

 Miili ya baadhi ya watu waliofunikwa na kifusi ikiwa inafanyiwa

utaratibu wa kwenda kuhifadhiwa.

 kamati ya ulinzi na usalama ilikuwepo.
 Greda ya manispaa ikijaribu kubeba gari lililoangukiwa na ngema ili

zoezi la uopoaji miiili  uendelee kwa urahisi.

 Miili ya  marehemu waliofukiwa na kifusi ikitolewa katika udongo baada ya kazi ya zaidi ya saa 5 ya kufukua eneo hilo kumalizika.
 Zoezi la kuopoa miili ya marehemu likiendelea.



 Baadhi ya ndugu wa marehemu walizimia baada ya kuona miili ya ndugu zao ikiopolewa kutoka kwenye udongo.

No comments:

Post a Comment

Pages