HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 20, 2013

OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI YAWANG'OA MAWAZIRI WANNE 
DODOMA, Tanzania
RAIS Jakaya Kikwete leo ametengua uteuzi wa mawaziri wanne waliotajwa na Ripoti ya Kamati Ndogo ya Bunge iliyoundwa kuchunguza madhila yaliyotokana na Operesheni Tokomeza Ujangili.

Mawaziri hao ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamisi Kagasheki; Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi; Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza baada ya wabunge kuchangia hoja hiyo iliyotikisa Bunge na kuleta simanzi kubwa kutokana na unyama uliofanywa dhidi ya wananchi ikiwemo kuuawa, kuteswa, kubakwa kwa wanawake pamoja na mifugo kuuawa, alisema alizungumza na Rais Kikwete na akasema anaungana na wabunge na kuagiza mawaziri hao wachukue hatua bila kujali wamehusika moja kwa moja au la.

Kabla ya kauli hiyo ya Pinda,  Bungeni mjini Dodoma leo jioni, tayari Waziri Kagasheki alitangaza kujiuzulu.
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki.
  Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.
 Aliyekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo.
 Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi.

No comments:

Post a Comment

Pages