Na
Elizabeth John
BAADA ya kutimiza miaka 15 tangu alipoingia katika tasnia ya
muziki ya Bongo Fleva, msanii Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ anatarajia kufuangua
studio ya kufanya kazi za ‘live’ na matangazo mbalimbali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Dully alisema, anaamini
studo hiyo itakuwa kati ya studio bora na zenye mvuto kutokana na umakini ambao
atakuwa nao.
“Sisemi kama Bongo hamna studio kubwa zipo lakini hii itakuwa
ndio namba moja, wanaopenda kufanya kazi na mimi na kutangaza biashara zao
karibuni sana, studio naihamishia Tabata Bima sio Kinondoni tena,” alisema.
Alisema, hivi karibuni anatarajia kutangaza siku ya kuanza
kufanya kazi hivyo wanaopenda kufanya nae kazi wakae mkao wa kula.
‘‘Nitaanza kufanya kazi na bendi mbalimbali, mtu
mwenyebiashara yake anataka matangazo nae namkaribisha kutekodi audio na video
kwa wasanii wenzangu na kazi zingine nyingi tu ni vizuri ufike ujionee
mwenyewe,” alisema.
Dully ni kati ya wasanii wa Bongo ambao wanafanya vizuri
kutokana na ubora wa mashairi ambayo yanakuwa na mvuto kwa jamii na kumtangaza
vema katika soko hilo.
No comments:
Post a Comment