MWANADADA anayetesa katika tasnia ya filamu nchini, Kajala Masanja, amesema kutokana na jinsi ambavyo ugomvi wake na aliyekuwa rafiki yake kipenzi, Wema Sepetu ulivyokuwa mkubwa, amefikia hatua anaiogopa simu yake na kutamani kuizima kila wakati.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kajala alisema, amekuwa akiumizwa na jinsi anavyotukanwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ugomvi huo.
Alisema ugomvi wake na Wema haujatokana na kile kinachodaiwa kuwa alimchukulia ‘bwana’ na kwamba umetokana na vitu vidogo ambavyo ni binafsi kwao na pia ugomvi huo unakuzwa zaidi na watu pamoja na vyombo vua habari kitu kinachopelekea wajikute maadui wa kweli.
“Kumekuwa na maneno na maneno kwamba mimi nimeanza kumchukia Wema baada ya kuona ameanza kuishiwa hela, lakini urafiki wagu mimi na Wema ulianza tangu hana kitu, sio kweli mimi siwezi kumfanyia Wema hivyo hela si kitu zaidi ya kitu,” alisema.
“Kiukweli kukosana na Wema inaniathiri sana kwasababu ni mtu ambaye nimemzoea mtu ambaye tumefanya vitu vingi kwahiyo muda mwingine nikikaa huwa namkumbuka sana,” alisema mrembo huyo.
Aliongeza kuwa ameshawahi kumtaka Wema wamalize ugomvi wao lakini ilishindikana japo amesema kwakuwa ugomvi ni wao wenyewe ipo siku utaisha na watakuwa marafiki tena kama ilivyokuwa hapo awali.
No comments:
Post a Comment