Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote katika uwanja wa ndege wa kiwanda chake cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014. Kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ishaya Samaila Majanbu. (Picha na Ikulu)
Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akipata maelezo toka kwa mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote wakati akizungushwa kuangalia kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos
Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akipata maelezo toka kwa mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote wakati akizungushwa kuangalia kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos
Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akipata maelezo toka kwa mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote wakati akizungushwa kuangalia kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kwenye machimbo ya kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kwenye mtambo wa kuzalisha umeme wa kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa aina ya mali ghafi inayotumika alipotembelea kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa na mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote kujionea maeneo mbalimbali ya kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika mfuko wa saruji alipotembelea kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa baada ya kutembelea kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014.
LAGOS, Nigeria
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametumia siku
nzima Ijumaa, Mei 9, 2014, kutembelea kiwanda kikubwa zaidi cha saruji kuliko
kingine chochote duniani cha Dangote Cement Obajana Plant na kinachomilikiwa na
tajiri mkubwa zaidi wa Afrika, Bwana Aliko Dangote, ambaye pia anajenga kiwanda
kikubwa cha saruji mjini Mtwara.
Akiandamana
na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Abdallah Kigoda, kwa siku nzima,
Rais Kikwete ametembelea kiwanda hicho cha Saruji cha Dangote kilichoko katika
eneo la Obajana, Jimbo la Kogi, kilomita 400 kaskazini mashariki mwa mji
maarufu wa kibiashara wa Nigeria, Lagos.
Rais Kikwete
ambaye alikuwa nchini Nigeria kuhudhuria Kongamano ya Uchumi Duniani-Afrika
(WEFA) mwaka huu aliamua kutumia siku yake ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu
nchini humo, kwa kutembelea uwekezaji mkubwa wa mwekezaji ambaye ameanza ujenzi
wa kiwanda cha saruji cha Mtwara ambacho kitakuwa kiwanda kikubwa zaidi cha
saruji kuliko kingine chochote katika Tanzania, kikiwa na uwezo wa kuzalisha
tani za kimetriki milioni tatu kwa mwaka.
Rais Kikwete
ambaye amepokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kiwanda hicho na Bwana Dangote
mwenyewe, ameanza ziara yake kwa kutembelea machimbo ya kiwanda hicho ambayo
yako kilomita tisa kutoka kiwandani ambako malighafi ya kiwanda hicho
husafirishwa kwa madaraja na mikada maalum hadi kiwandani.
Bwana
Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kwa sasa Kiwanda cha Obajana kinazalisha
tani za kimetriki milioni 10.25 kwa sasa kwa mwaka na hivyo kukifanya kiwanda
hicho kuwa kiwanda kikubwa zaidi cha saruji duniani kilichoko katika eneo moja
na kuwa baada ya upanuzi unaoendelea kufanywa kwenye kiwanda hicho, uwezo wake
wa uzalishaji utaongezeka na kufikia tani za kimetriki 13.0 kwa mwaka ifikapo
mwakani 2015.
Bwana
Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kiwanda hicho kilicho kwenye eneo la
kilomita za mraba saba kitakuwa kimegharimu kiasi cha dola za Marekani bilioni
2.5 wakati upanuzi wake utakapokamilika. Kwa sasa kiwanda hicho kina biashara
ya dola za Marekani bilioni mbili kwa mwaka.
Bwana
Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kiwanda hicho kilichoanza kujengwa mwaka
2003 na kukamilishwa mwaka 2006 na hatimaye kuzinduliwa na Rais Olusegun
Obasanjo Mei 12, mwaka 2007, wiki mbili kabla ya kustaafu Urais wa Nigeria,
kinaajiri watu 800 kwa wakati mmoja na hivyo kuwa miongoni mwa waajiri wakubwa
zaidi katika Nigeria.
“Mheshimiwa
Rais, ili kuelewa vizuri mchango wa kiuchumi na kijamii za kiwanda hiki na
viwanda vyetu vingine katika maeneo mengine ya Nigeria, unahitaji kukumbuka
kuwa kabla ya kuanza kujenga kiwanda hiki, Nigeria nzima ilikuwa na uwezo za
kuwazalisha tani za kimetriki za saruji milioni1.5 tu, wakati huo chini ya
miaka 10 iliyopita. Tunataka kufikia hatua ya kuhakikisha kuwa eneo la Afrika
Magharibi na hata Bara letu la Afrika linaacha kabisa kuagiza saruji nje ya Bara
letu. Na tutafikia huko.”
Mbali na
Kiwanda cha Obajana, Kampuni ya Saruji ya Dangote inazalisha saruji katika
maeneo mengine mawili ya Nigeria ambalo uzalishaji wa jumla wa maeneo hayo
matatu ni tani za metriki 20.25 kwa mwaka.
Amesema
Bwana Dangote kuwa ili kuweza kuwa na uhakika wa umeme, uongozi wa kiwanda
hicho uliamua kuzalisha umeme wake kwa ajili ya kiwanda hicho kwa kujenga,
miongoni mwa hatua nyingine, bomba ya kilomita 92 la kusafirisha gesi kutoka
Ajaokuta hadi kwenye kiwanda hicho.
Alipoulizwa
na Rais Kikwete kama wanategemea kwa namna yoyote umeme wa taifa, Bwana Dangote
alijibu kwa furaha, “hatujaunganishwa kwenye gridi ya taifa na tunadhani hili
ni jambo zuri kwa sababu hatua tulizochukua zinatuhakikishia umeme wakati wote
na kwa kiwango ambacho tunakihitaji. Tunatumia gesi ama diseli yetu wenyewe. Na
wala siyo umeme tu, hata miundombinu ya eneo hilo kiliwemo daraja hili kubwa
linalonganisha eneo la machimbi na kiwanda, tumejenga sisi Mheshimiwa Rais.”
Bwana
Dangote amesema kuwa mbali na kujenga miundombinu ya umeme wake, kiwanda hicho
pia kimejenga bwawa lake lenyewe kwa ajili ya huduma ya maji kusaidia
uzalishaji wa saruji bila kutegemea huduma ya maji ya Serikali. Aidha, bwawa
hilo linatoa huduma ya maji kwa jamii inayozunguka kiwanda hicho.
Mbali na
shughuli za kiwanda, Kampuni ya Bwana Dangote inashiriki kwa karibu sana
shughuli za jamii inayozunguka kiwanda ambacho kwa sasa imeanzishwa miji midogo
saba katika eneo lililokuwa pori lenye nyumba 50 za wenyeji tu kabla ya
shughuli za kiwanda hicho kuanzishwa.
Bwana
Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kampuni yake inatoa shughuli za elimu,
maji na umeme kwa wananchi ambao wanazunguka kiwanda ambacho tokea kuanzishwa
kwake limevutia mabenki 13 ambayo yameanzishwa matawi yake katika eneo la
kiwanda. “Mheshimiwa Rais, mbali na nyumba za wafanyakazi, tunawajengea hata
nyumba za kuishi wananchi wanaozunguka eneo hili ambao wanatuunga mkono sana.”
Mbali na
kutoa huduma nyingine za kijamii, Kampuni ya Saruji ya Dangote inajenga taasisi
kubwa ya elimu ya Dangote Academy ambayo itatoa elimu na mafunzo ya kiufundi
kwa ajili ya kuandaa wafanyakazi wa kiwanda hicho na watoto wa jamii
inayozunguka kiwanda hicho.
Ili
kuhakikisha kuwa upanuzi wa kiwanda hicho unakwenda kwa kasi kubwa zaidi, Bwana
Dangote ameagiza kiasi cha malori 6,000 kutoka China kusaidia ujenzi na pia
amechukua uamuzi usiokuwa wa kawaida wa kuagiza maelfu ya vibarua kutoka nchi
hiyo hiyo ya China kushiriki katika ujenzi huo na kuumaliza kwa haraka.
Bwana
Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kampuni yake inafanya jitihada kubwa
kuhakikisha kuwa Rais Kikwete anakifungua kiwanda cha saruji cha Mtwara
kabla ya kustaafu mwishoni mwa mwaka ujao.
Mbali na
Nigeria na Tanzania, Bwana Dangote ana viwanda ama anajenga viwanda vya saruji
ama na shughuli za saruji katika nchi 14 za Afrika ikiwamo Ethiopia, Zambia,
Mozambique, Kenya, Senegal na Sierra Leone, Afrika Kusini, Congo (Brazzaville),
Cameroun, Ghana, Liberia na Ivory Coast.
Mbali na
shughuli za uzalishaji wa saruji, Bwana Dangote ambaye anakubaliwa kuwa tajiri
mkubwa zaidi katika Afrika kwa thamani ya dola za Marekani bilioni 25 yeye na
kampuni yake ya Dangote Group pia ina shughuli za uzalishaji wa sukari,
uzalishaji wa chumvi, utengenezaji wa magunia, uzalishaji maji, uzalishaji wa
vyakula vya aina mbali mbali, uzalishaji wa mafuta ya kupikia, utengenezaji wa
nyanya. Kwa sasa anaendelea na ujenzi wa kiwanda cha mbolea na kile cha
kuzalisha bidhaa za petrol na kemikali.
Kampuni ya
Saruji ya Dangote – Dangote Cement- ndiyo kampuni kubwa kuliko zote katika
Afrika Magharibi kwa sasa ikiwa na thamani ya dola za Marekani bilioni 22.7 kwa
tathmini ya mwaka huu baada ya kuongeza thamani yake kutoka dola za Matrekani
bilioni14.5 za mwaka jana.
Mwishoni mwa
ziara hiyo yenye mafanikio makubwa, Rais Kikwete ameondoka Obajana kurejea
nyumbani kupitia Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Luanda, Angola
ambako kesho (jumamosi) anatarajia kukutana na marais wa nchi hiyo kabla ya
kurejea nyumbani.
No comments:
Post a Comment