Na Elizabeth John
MKALI wa hip hop nchini, Farid Kubanda ‘Fid Q’
amesema asilimia kubwa ya misemo ya mashairi yake huwa anaitoa kwa babu yake na
baadhi ya vitabu vya hadithi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Fid Q
alisema, babu yake ni muongeaji sana na akikaa naye kuwa anakariri maneno mengi
ambayo yanamsaidia katika utunzi wa mashairi yake.
“Babu yangu amenisaidia sana mpaka kufika hapa,
namsdhukuru sana, pia msanii umatakiwa kusoma vitabu mbalimbali ili kupata
baadhi ya maneno ambayo yataleta vionjo katika mashairi yako,” alisema.
Fid Q alisema kwasasa yupo katika mikakati ya
kuandaa kazi yake mpya ambayo anaamini itakuwa moto wa kuotea mbali kutokana na
mashairi ambayo yapo ndani yake.
Msanii huyo ni kati ya wasanii wakongwe ambao
wanatamba katika tasnia hiyo akiwa na kazi zake kama ‘Agosti 13’, ‘Siri ya
Mchezo’, ‘Mwanza Mwanza’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya
vizuri.
No comments:
Post a Comment