STAA wa filamu za Bongo, Riyama Ally amesema lugha
ya Kingereza ni tatizo kubwa kwa wasanii wa Bongo inayopelekea kushindwa
kutamba kimataifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Riyama
alisema hakuna mtu ambaye atapingana nay eye kwa hilo, wasanii wengi wamekuwa
wakifanya vizuri hapa nchini lakini wanapokwenda huko wataboronga.
“Mimi binafsi ukinipeleka nchi za watu hakika
utakuwa na kazi ya ziada ya kunifafanulia anachokiongea, wengi sio wawazi mimi
siwezi kucheza na mtu anayeongea lugha nyingine nitawasiliana nae vipi sasa,”
alisema Riyama.
Aidha, Riyama alisema kwasasa akitokea mtu
anayetaka kumsomesha ili kuendeleza kipaji chake yupo tayari wakati wowote na
anahamu ya kujua lugha nyingine.
Riyama ni kati ya walimbwende wanaotamba katika
tasnia ya filamu nchini huku akishiriki filamu nyingi zikiwemo, Kigodoro, Tabu
ya kuoleana, Fungu la kukosa, Wrong Number na nyinginezo nyingi ambazo
zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia hiyo.
No comments:
Post a Comment