Ofisa Mwandamizi wa NSSFkutoka Kitengo cha Hiari Scheme, Salim akiwa na cheti cha ushiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajasiriamali wanawake alichokabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kulia), wakati wa kufunga mafunzo hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa.
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limewataka watanzania kutumia fursa
zinazotolewa na mfuko huo ili kujikwamua kiuchumi kwa kupata akiba ,
mafao na mikopo itakayo kuwa sawa na watu walioajiriwa.
Akitoa rai hiyo jijini Dar es Salaam, Ofisa Mwandamizi kutoka Kitengo cha Hiari
Scheme, Salim Kimaro wakati wa Kufunga Mafunzo ya kuwajengea uwezo
wanawake wajasiriamali waliotoka katika mikoa yote ya Tanzania.
Alisema kuwa, ili kuhakikisha kila mtu
anafaidika na mfuko huo wamelenga kupanua wigo kwa watanzania wote ili
wanufaike na huduma wanazotoa ikiwemo Pensheni, mafao ya mtibabu na uzazi kama
ilivyo kwa watu walioajariwa.
“Nchi
yetu inakadiriwa kuwa na watu Millioni 44, ambapo nguvu kazi ya watu wa umri
kati ya miaka (15-60) ni million 22.7, kati yao million 1.2 tu ndio
wanahudumiwa na mfuko wa Hifadhi ya Jamii, hii inamaanisha watu
million 21.6 ndio walioko katika ajira binafsi na hawafikiwi na Mfuko wa
hifadhi ya Jamii hivyo tumeona ni bora kuhusisha sekta binafsi ili kuwakomboa
watanzania”
Alifafanua
sababu ya kuhusisha sekta binafsi katika hifadhi ya jamii kuwa ni, kutoa
mafao yote yanayotolewa na NSSF, kusaidiana na serikali kupunguza umasikini,
kuwajengea uwezo wajasiriamali kwa kuwapa mikopo, kuwapa wanachama huduma ya
matibabu bure ili waweze kupata afya na kuendelea kuzalisha mali.
“Ili
kuwa mwanachama wa hiyari unashahuriwa kwenda ofisi yoyote ya NSSF
iliyo karibu nawe isipokuwa makao makuu, ambapo mtu anatakiwa kutoa tamko la
kipato chake kwa mwezi ili kutoa asilimia 20, pia mwanachama wa hiyari au sekta
binafsi atapaswa kulipa kiwango chochote kisiwe chini ya sh 20, 000 kila mwezi”
Kimaro alisema kuwa miongoni mwa faidia na mambo muhimu watakayowanufaisha
wanachama ni kutoa mikopo ya elimu, uendelezaji wa biashara na kuboresha
makazi, matibabu ya bure kwa wanachama na familia zao (mke, mume na watoto wane
wa chini ya miaka 18-21 iwapo wako shule).
Aliongezea
kuwa “Mwanachama wa hiari anayo haki ya kupata mafao yote saba yatolewayo na
NSSF kwa mujibu wa sheria, mafao hayo ni ya muda mrefu yaani Pensheni ya uzee,
urithi na ulemavu na mafao ya muda mfupi ambayo ni matibabu, uzazi,
kuumia kazini na msaada wa mazishi”
No comments:
Post a Comment