HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 20, 2014

Agizo la JK lawatupa rumande wananchi Gairo

Na Bryceson Mathias, Gairo

WANANCHI wa Wilaya ya Gairo, wamelalamikia agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuzitaka Halamashauri Kujenga Maabara za Shule za Sekondari, kuwa limeanza kuwa Mwiba ambapo wasiochangia Shilingi 10,000/- wanatupwa rumande na watendaji.

Katika Mchango huo, kwenye kila Kaya Baba, Mama na kila Mtoto aliyefikisha umri wa  Miaka 18 anatakiwa kuchangia Shilingi 10,000/- na kuanzia leo Jumamosi, Julai 19, mwaka huu kuna patashika nguo kuchanika na anayeshindwa anatupwa rumande.

Diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Gairo, Dustan Mwendi, amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema, hayo yalikuwa ni makubaliano ya Kikao cha Madiwani kilichofannyika na kuridhiwa na Kiogozi wa Mkoa, Joel Bendera,anashangaa katika Utekelezaji linapingwa.

“Ni kweli mwandishi tukio la kamata kamata kwa asiyelipa linafanyika watendaji wanatekeleza makubaliano tuliyokubaliana, lakini tunashangaa ndugu zetu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwemo viongozi wakuu hapa wilayani wamekuwa wa kwanza kupinga nadhan ni siasa.

“Maeneo yetu ya Chadema tayari wameshalipa hadi kufikia Milioni 7/- lakini kwa wenzetu wameanza kupinga na kuna taarifa kuna vikao vya Kamati ya siasa vimekaa huenda ndio sababu ya upinzani huo”.alisema Diwani Mwendi.

Kwa Sensa ya 2012 ya watu wazima tarafa ya Gairo inaonesha ina watu 45,000 hivyo kuna uwezekano wa kukusanya Milioni 450/- ambazo wananchi wanadai fedha hizo hazitatumika kujengea Maabara ila zitawekwa mahali kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Aidha Walipoulizwa mbona Diwani wao ni wa Chadema ambaye hawezi kuacha wadhulumiwe na fedha hiyo kutotumika vibaya walidai, katika hali tatanishi, hata wao CCM sasa hivi wamechoshwa na vitendo vya Ufisadi na Dhuluma, hivyo Diwani hajui atazungukwa tu.

No comments:

Post a Comment

Pages