NA ELIZABETH JOHN
STUDIO ya Bongo Rekord iliyo chini ya
mtayarishaji mkongwe nchini, P Funk Majani natafuta wasanii wapya wenye
vipaji ikiwa ni pamoja na wale wanaojijua kama wanabahati.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,
Majani alisema anatafuta wasanii watano ambao watafanya kazi chini ya label ya
Bongo rekodi kwa upade wa wanawake na wanaume.
Alisema, anataka kuchanganya pamoja ili
atengeneze kundi ambalo atatangaza nia yake hapo baadae, kwa wasanii wa bongo
fleva, hip hop na watayarishaji.
“Hao wote watakuwa kwa label ya bongo
rekodi ambayo ilikuwepo zamani ikijengwa na wasanii mbalimbali sasa hivi
tumerudi tena kwa lengo la kukuza muziki wetu,” alisema.
Majani alisema kwa yeyote ambaye anataka
kuwa chini ya label hiyo anatakiwa kutuma kazi zake kwenye bongo_recordz@yahoo.com ili
kumuwezesha yeye kuona kazi za msanii huyo.
Mwisho.




No comments:
Post a Comment