Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa filamu na
muziki kutoka Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa
wasanii wa
Tanzania. Wasanii hao ni na Terrence J. Jenkins, mwendeshaji wa
kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment (wa pili
kulia) Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya
Disturbing The Peace Records (wa pili kushoto) na Davis Banner, mwigizaji,
mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda
tuzo maarufu ya Grammy.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitumia simu yake ya mkononi kuwaonesha
vivutio vya kitalii wasanii nyota wa muziki na filamu wa Kimarekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa
mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni Terrence
J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E!
Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton,
Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media
Group. Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka
Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki,
mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu
ya Grammy.
PICHA NA IKULU.
xxxxxxxxxxxxxxxx
xxxxxxxxxxxxxxxx
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete Jumatatu Julai 14, 2014 amekutana na kundi la wasanii kutoka
Marekani lililowasili nchini usiku wa Alhamisi, Julai 10, 2014, kwa ajili ya
kuendesha mafunzo kwa wasanii wa Tanzania kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya
Tanzania (BOT) mjini Dar es Salaam.
Wasanii hao ni pamoja na Terrence J. (Jenkins),
mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji
wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki
katika Kampuni ya Outlet Media Group.
Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka
Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki,
mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu
ya Grammy.
Kiasi cha wasanii 250 walishiriki semina hiyo inayoitwa
Mafunzo ya Uendelezaji Usanii. Hiyo ilikuwa ni kutimiza ahadi aliyotoa Rais
Kikwete kwa wasanii wa Tanzania kuwa atachangia kuinua kiwango cha ujuzi na
weledi wao kwa kuwaandalia mafunzo yatayoendeshwa na magwiji wa sanaa kutoka
Marekani sasa imetimia.
Akizindua Kampeni ya Uzalendo kwa Vijana inayoendeshwa na
Muungano wa Wasanii Tanzania kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma mwezi
uliopita, Juni 14, 2014, Rais Kikwete aliahidi kuchangia kuinua kiwango cha
usanii na weledi wa wasanii wa Tanzania kwa kusaidia kuandaa mafunzo
yatakayoendeshwa na wasanii maarufu kutoka Marekani.
Mbali na kuendesha shughuli za mafunzo ya wasanii ambazo
wamekuwa wakizifanya kwa makundi madogo madogo tokea walipowasili nchini, pia
wanamuziki hao wa Marekani na kundi la wapiga picha watatembelea sehemu mbali
mbali nchini, hasa kwenye vivutio vya watalii, ambako watapiga picha na
kuandaa vipindi vya kuitangaza Tanzania katika vyombo vya habari vya Marekani.
Imetolewa
na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
15
Julai,2014
No comments:
Post a Comment