Na Keneth Ngelesi, Rungwe
WANANCHI
waishio katika vijijini vilivyopo kando kando ya lango kuu la kuingilia Mlima Rungwe wameashwa kuwatumia watalaamu waliopo katika
ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya kubuni na
kuibua miradi ya kuichumi ambayo ni rafiki wa mazingira.
Hayo
yalibainishwa hivi karibuni na Festo Sikagonamo Mkurugenzi wa shirika lisilo la
kiserikali linajuhusha na uhifadhi wa Mazingira Elimisha wakati wa kutoa elimu
ya ufungaji wa nyuki kwa njia ya kisasa kwa wananchi ya kijiji cha Syukula
Wilayani hapa.
Akizungumza
na wananchi hao Sikagonamo aliwataka kuwa wabunifu hasa katika uibuaji wa miradi
ambayo ya kujikwamua kiuchumi wakati huo huo ikawa ni njia moja wapo ya
kuifadhi mazingira ambayo kwa hivi sasa
yameanza kuharibiwa.
Alisema kuwa
taasisi hiyo imeamua kujikita zaidi kutoa elimu ya ufugaji wa nyuki kutokana
miradi hiyo kuitaji mtaji mdogo na kwamba mwanachi wa kawaida anaweza kumudu huku akiwa anashirika kampeni
za uifadhi wa mazingira.
Alisema kuwa
endapo wananchi hao wataitikia mwito huo wanaweza kuondokana na umasikini kwani
soko la bidhaa zinazo tokana na nyuki ikiwemo asali ni kubwa ndani ndani na nje ya nchi.
Aliongeza
kuwa mbali la soko la ndani lakini pia bidha hizo ambazo ni pamoja asali
inaweza kuuzwaasa kwa watalii ambao wamekuwa wakifika katika mlima huo na vivutio vingene vilivyopo
katika Wilaya hiyo na Mkoa kwa ujumla.
Alisema kuwa
Wilaya ya Rungwe imejaliwa uoto wa asili mzuri na rafiki kwa ufugaji wa nyuki na kwamba wakazi katika Wilaya hiyo hawajazitumia vyema fursa
zilizopo, ambapo zingetumika vyema umasikini kwa wananchi wa Wilaya hiyo
ingekuwa ni hadidhi.
Kwa upande
wake Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Busokela Wilaya ya Rungwe Anamary Joseph ambaye ni miongoni mwa
watalaamu walio fundisha mada mbalimbali za ufugaji wa nyuki na uhifadhi wa
mazingira aliwataka wananchi wa kijiji hicho walio shiriki mafunzo hayo kuwa
mabalozi kwa wale walioshindwa kushiriki mafunzo hayo.
Aidha alisema
kuwa ni vema wananchi hao wakaanzisha miradi hiyo kupitia vikundi na kwamba
taasisi ya Elimisha kushirikiana na Serikali watakuwa tayari kutoa mitaji kwa pamoja
na kutoa vifaa kwa ajili ya miradi hiyo.
Afisa huyo
alibainisha vifaa ambavyo vimesha nunuliwa na vinasubiriwa kugawia kwa vikundi
ambavyo vitakuwa vipo trayari kuanzisha mradi wa ufugaji wa nyuki ni
Masanduku,kwa ajili ya Mizingi, na vifaa vingine pam oja na kuwa taftia soka na
bidhaa zitokanazo na ufugaji nyuki.
Akitoa
shukurani kwa niaba ya wananchi walioshiriki Mafunzo hayo Mwenyekiti wa kamati
ya Mazingira kijiji hapo Dickson Mwamakula alishukuru hatua ilichulkulia na
Tasisi hiyo ya mazingira na kwamba elimu hiyo imefika mwafaka na imepokelewa
kwa Mikono miwili.
Alisema kuwa
wananchi wengi wamekuwa wakichukulia nyuki kama adui lakini kwa elimu iliyo
tolewa na wataalamu wanaamini kabisa itasaidi kuondoka na umasikini kwani mchanganuo
uliotolewa unaonyesha wazi nyuki mazao yatokanayo na nyuki yakitumika vyema
yanaweza kuwa sadia wananchi kupiga teke umasikini.
No comments:
Post a Comment